TAZAMA MAJEMBE MAPYA YA SIMBA YALIVYOTAMBULISHWA KWA MKAPA, JEAN BALEKE, ISMAEL SAWADOGO WOTE NDANI KABLA ya kuanza kwa mchezo wa ligi kuu bara kati ya Simba vs Mbeya City katika dimba la Mkapa, wachezaji wapya wa simba waliosajiliwa dirisha dogo wametambulishwa kwa mashabiki na kisha kukaa jukwaani kuutazama mchezo huo.
#NelsonOkwa #UsajiliSimba #Kiungo Ukiona Manyoya Ujue kuku Kaliwa; Hivi ndivyo unavyoweza kusema juu Usajili wa Nelson Esor BULUNWO OKWA, Mnigeria mwenye Miaka 25 anayekicheza katika nafasi ya Kiungo. Okwa kabla ya kutua Msimbazi alikuwa akikipiga na klabu ya Rivers United ya Nchini Nigeria; Ile iliyowatoa Yanga katika hatua ya Mchujo Klabu Bingwa Afrika Msimu Uliopita. Okwa ni miongoni mwa Wachezaji wachache Saaa katika Ligi yetu watakao tumia Miguu yote kusakata Kabumbu. Takwimu za ligi kuu nchini Nigeria zinaonyesha kuwa Okwa Msimu huu amecheza dakika 1731 katika mechi 26 kati ya 38, ikiwa ni sawa na wastani wa kucheza dakika 66.5 kwa kila mechi na kufanikiwa kucheka na Nyavu Mara 5. Labda nikiri tu kuwa Okwa ni miongoni mwa wachezaji Machachari sana wawapo Dimbani. KUpitia Uchambuzi huu nitakwambia Okwa ni Mzuri Zaidi akicheza Nafasi gani akiwa Uwanjani, lakini pia Nitakwambia kwa Simba ya Zoran, Okwa ili awe na Thamani anatakiwa kuchezeshwaje. Usisahau kupitia Hapa Nitakupa Picha halisi ya Vita ya Namba ninayoiona kutokana na Usajili wa Okwa Msimbazi. Kaa hapo hapo, tena kwa Kutulia na Ili Kuhakikisha kuwa hupitwi na chochote Nakuomba SUBSCRIBE kisha Bofya alama ya kengele; SoccerData imejipanga kukushushia Mawe ya Kiufundi na kuisogeza Timu yako karibu nawe. Tufuate kule Instagram na Facebook kwa Jina la SoccerdATA Tanzania. Bila kupoteza muda acha tuanze;
Fiston Kalala Mayele amefunga goli la ushindi kwa mtindo wa aina yake na kuifanya Yanga iondoke na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Azam FC kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi. Azam ndiyo waliotangulia kupata bao kupitia kwa Rodgers Kola kabla ya Yanga kusawazisha kwa penati kupitia kwa Djuma Shabani na kisha Mayele kupachika bao la pili dakika ya 78.
Benjamin Asukile ametokea benchi na kuifungia Tanzania Prisons mabao mawili yaliyoipa ushindi wa 3-2 dhidi ya Dodoma Jiji FC katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa leo kwenye Dimba la Sokoine, jijini Mbeya. Dodoma Jiji ndiyo waliotangulia kufunga kupitia kwa Anuary Jabir dakika ya 6, kabla ya Jumanne Elifadhili kusawazisha dakika ya 18 na kisha Dodoma kufunga la pili dakika ya 33 kupitia kwa Salmin Hoza.
Timu ya taifa ya Tanzania #TaifaStars imelazimishwa sare ya bao 1-1 na Sudan katika mchezo wa kirafiki uliopigwa leo kwenye Dimba la Benjamin Mkapa, Dar es Salaam. Sudan wametangulia kupata bao dakika ya 2 kupitia kwa Saddiq Toto na kisha Tanzania kusawazisha dakika ya 79 kupitia kwa Saimon Msuva.
Timu ya taifa ya Tanzania #TaifaStars imelazimishwa sare ya bao 1-1 na Sudan katika mchezo wa kirafiki uliopigwa leo kwenye Dimba la Benjamin Mkapa, Dar es Salaam. Sudan wametangulia kupata bao dakika ya 2 kupitia kwa Saddiq Toto na kisha Tanzania kusawazisha dakika ya 79 kupitia kwa Saimon Msuva.
NAMUNGO vs AZAM: Nyota wa Azam FC, Prisons Dube amefunga goli lake la kwanza kwenye ligi msimu huu, akiiongoza timu yake kuifunga Namungo FC mabao 2-1 ugenini. Katika mchezo wa #NBCPremierLeague uliopigwa leo kwenye Uwanja wa Ilulu mkoani Lindi, Namungo wametangulia kupata bao kupitia kwa Mohamed Issa Banka lakini Azam wakachomoa kwa goli la Prince Dube na kisha kupiga la pili kupitia kwa Ismail Aziz Kader.
Azam FC imepata ushindi wa mabao 2-1 ugenini dhidi ya Namungo FC, katika mchezo wa ligi kuu ya NBC uliopigwa leo kwenye Uwanja wa Ilulu mkoani LIndi. Namungo wametangulia kupata bao kupitia kwa Mohamed Isssa Banka lakini Azam wakachomoa kwa goli la Prince Dube na kisha kupiga la pili kupitia kwa Ismail Aziz Kader.