Content removal request!


NELSON OKWA: KIUNGO BUIBUI | UBORA | UDHAIFU | VITA MSIMBAZI.

#NelsonOkwa #UsajiliSimba #Kiungo Ukiona Manyoya Ujue kuku Kaliwa; Hivi ndivyo unavyoweza kusema juu Usajili wa Nelson Esor BULUNWO OKWA, Mnigeria mwenye Miaka 25 anayekicheza katika nafasi ya Kiungo. Okwa kabla ya kutua Msimbazi alikuwa akikipiga na klabu ya Rivers United ya Nchini Nigeria; Ile iliyowatoa Yanga katika hatua ya Mchujo Klabu Bingwa Afrika Msimu Uliopita. Okwa ni miongoni mwa Wachezaji wachache Saaa katika Ligi yetu watakao tumia Miguu yote kusakata Kabumbu. Takwimu za ligi kuu nchini Nigeria zinaonyesha kuwa Okwa Msimu huu amecheza dakika 1731 katika mechi 26 kati ya 38, ikiwa ni sawa na wastani wa kucheza dakika 66.5 kwa kila mechi na kufanikiwa kucheka na Nyavu Mara 5. Labda nikiri tu kuwa Okwa ni miongoni mwa wachezaji Machachari sana wawapo Dimbani. KUpitia Uchambuzi huu nitakwambia Okwa ni Mzuri Zaidi akicheza Nafasi gani akiwa Uwanjani, lakini pia Nitakwambia kwa Simba ya Zoran, Okwa ili awe na Thamani anatakiwa kuchezeshwaje. Usisahau kupitia Hapa Nitakupa Picha halisi ya Vita ya Namba ninayoiona kutokana na Usajili wa Okwa Msimbazi. Kaa hapo hapo, tena kwa Kutulia na Ili Kuhakikisha kuwa hupitwi na chochote Nakuomba SUBSCRIBE kisha Bofya alama ya kengele; SoccerData imejipanga kukushushia Mawe ya Kiufundi na kuisogeza Timu yako karibu nawe. Tufuate kule Instagram na Facebook kwa Jina la SoccerdATA Tanzania. Bila kupoteza muda acha tuanze;