Benjamin Asukile ametokea benchi na kuifungia Tanzania Prisons mabao mawili yaliyoipa ushindi wa 3-2 dhidi ya Dodoma Jiji FC katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa leo kwenye Dimba la Sokoine, jijini Mbeya. Dodoma Jiji ndiyo waliotangulia kufunga kupitia kwa Anuary Jabir dakika ya 6, kabla ya Jumanne Elifadhili kusawazisha dakika ya 18 na kisha Dodoma kufunga la pili dakika ya 33 kupitia kwa Salmin Hoza.