Leo tarehe 07/04/2023 ni Siku kubwa kwa Wana Michezo Tanzania hususani upande wa Soka ambapo kunapigwa Mchezo wa hatua ya Robo Fainali Kombe la Azam Sports Federation Simba dhidi ya Ihefu, Mshindi anakwenda Nusu Fainali kukutana na Azam FC. Mchezo huu unapigwa majira ya saa moja kamili za Usiku kwenye Dimba la Azam Complex. Mpenja Tv tumefika mapema kukuhabarisha kabla na baada ya Mchezo.
Baada ya kushuhudia Mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika Tp Mazembe dhidi ya Yanga uliopigwa kwenye ardhi ya Congo leo tarehe 02/04/2023. Ghalib Mzinga "Kilwa Finest" Ametoa Tathmini yake mapema baada ya Mchezo kumalizika, ameeleza Ubora wa Yanga kwenye Mchezo huo na Ubora wa Vikosi vilivyoanza. Aidha Mzinga amechagiza kuwa ameiona Yanga Kikosi cha kwanza dhidi ya Mazembe nyingine.
Leo March 19 2023,Yanga SC anamkaribisha US Monastir kutoka Nchini Tunisia Katika Dimba la Benjamin Mkapa,kwenye Mchezo wa Kundi D wa Kombe la Shirikisho Afrika, Mchezo Unaochezwa Saa Moja Jioni
Moto Utawaka Uwanja wa Benjamin Mkapa ni Mchezo Mkubwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Simba Sc dhidi ya Horoya AC Majira ya Saa 1:00 Jioni. Mpenja Tv tunahakikisha tunakuletea Mfululizo wa Matukio yote yanayohusu Mechi hiyo Kabla na Baada ya Mechi.
Hii ni kutoka Ulipo Uwanja wa Azam Complex,Chamazai ambako inachezwa Mechi ya Ligi Kuu ya NBC kati ya Yanga Sc ambao ni Wenyeji wa Mechi hiyo wakiikaribisha Geita Gold. Na hivi ndivyo Hali ilivyo Nje ya Uwanja huo,Kupitia Mpenja Tv tunahakikisha tunakuletea Mfululizo wa Matukio ya Kabla na Baada ya Mechi hiyo
Leo March 08 2023,Yanga SC anamkaribisha AS Real Bamako kutoka Nchini Mali Katika Dimba la Benjamin Mkapa,kwenye Mchezo wa Kundi D wa Kombe la Shirikisho Afrika, Mchezo Unaochezwa Saa Moja Jioni.
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC ,Ahmed Ally amezungumzia maandalizi yao ya Mchezo wa kesho wa kombe la Shirikisho la Azam Sports hatua ya 16 Bora dhidi ya African Sports ,Utakaochezwa Uwanja wa Uhuru,Saa 10 Jioni.
Yanga SC wamewasili Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere wakitokea Nchini Mali,ambapo Siku ya Jumapili ya Januari 26 walicheza Mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya Makundi dhidi AS Real Bamako,Mchezo uliyokwisha kwa Sare ya 1-1.