Azam FC's user profile page. Match highlights, posts and more on site!

“”

 Report User

Highlights

Waziri Mwakyembe aimwagia sifa Azam FC; Asema ni Kiwanda cha Soka Tanzania
Waziri Mwakyembe aimwagia sifa Azam FC; Asema ni Kiwanda cha Soka Tanzania

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwankyembe, leo alifanya ziara ya kutembelea Makao Makuu ya Azam FC ‘Azam Complex’ na kukiri kuwa timu hiyo ni kiwanda cha soka nchini. Ziara hiyo ya Mwakyembe ilikuwa ni maalumu kwa ajili ya kuangalia Azam FC ilipofikia kwenye uboreshaji wa uwanja huo ikiwa ni maandalizi ya kuelekea fainali za Mataifa ya Afrika kwa Vijana chini ya umri wa miaka 17 (AFCON U-17) zitakazofanyika nchini mwakani. Uwanja wa Azam Complex ni miongoni mwa viwanja vitatu nchini vilivyoteuliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kwa kushirikiana na la hapa nchini (TFF), vingine viwili vikiwa ni Uwanja wa Taifa na ule wa Uhuru. Kigogo huyo aliambatana na Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo Taifa (BMT), Alex Nkeyenge na Mkurugenzi wa Mashindano TFF, Salum Madadi, ambao walikaribishwa na wenyeji wao akiwemo Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Wakurugenzi, Nassor Idrissa ‘Father’, Makamu Mwenyekiti Omary Kuwe, Meneja wa timu, Philllip Alando. Akitoa neno kwenye ziara hiyo, Waziri Mwakyembe, aliupongeza uongozi wa Azam FC kwa kazi kubwa waliyofanya kwenye kuboresha uwanja huo kwa ajili ya fainali hizo ambazo zitafanyika kwa mara ya kwanza nchini. “Kwa kweli ni mara yangu ya kwanza kutembelea Azam Complex na nimejiridhisha mwenyewe kwamba hiki ni kiwanda cha soka, kiwanda cha michezo kuna kila kitu hapa na tukifikia hatua ambayo pengine timu zetu zenye sura ya Kitaifa hata zikawa tatu, nne, tano zikawa na mfumo ulioko hapa Azam Complex tayari sisi Tanzania tumeshakuwa nchi ya soka. “Na nadhani tutaanza kuuza wachezaji wengi sana duniani ambao pia watachangia sana katika pato la Taifa maana wenzetu wengi kama nchi ya Brazil inaendeshwa na pesa kama hiyo, Azam hongereni sana mmefanya kazi kubwa sana,” alisema.



Ngoma awaahidi makubwa mashabiki Azam FC | Ngoma First Action At Azam FC
Ngoma awaahidi makubwa mashabiki Azam FC | Ngoma First Action At Azam FC

BAADA ya jana kucheza mechi yake ya kwanza Azam FC akitokea kwenye majeruhi, mshambuliaji Donald Ngoma, ameonesha kufurahishwa sana huku akiwaahidi makubwa mashabiki wa timu hiyo. Azam FC iliyokuwa ikicheza na Lipuli jana usiku na kutoka suluhu, ilishuhudiwa Ngoma akiingia dakika ya 62 kuchukua nafasi ya kiungo mkabaji Mudathir Yahya, mchezo huo pia ukiwa ni wa kwanza kwake tokea asajiliwe na timu hiyo msimu huu akitokea Yanga. Licha ya kutoka kwenye majeraha ya takribani mwaka mmoja, Ngoma alionekana kuanza vema jana mechi yake ya kwanza akicheza kwa kujituma na kupambana na mabeki wa Lipuli huku akipata nafasi muhimu mbili za kufunga moja ikiwa ni ile ya kuangushwa katika eneo la hatari na kipa.



Mzungu apagawishwa na Azam FC na kujiunga na mashabiki kushangilia ushindi
Mzungu apagawishwa na Azam FC na kujiunga na mashabiki kushangilia ushindi

Mzungu apagawishwa na Azam FC na akijiunga na mashabiki wa timu hiyo mara baada ya ushindi dhidi ya Alliance (1-0) juzi. Shuhudia uhondo kamili kwa kuangalia video hii.



AZAM FC U-20 OFF TO DODOMA | Uhai Cup U-20 2018 | June 7, 2018
AZAM FC U-20 OFF TO DODOMA | Uhai Cup U-20 2018 | June 7, 2018

KIKOSI cha timu ya vijana ya Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Azam FC U-20, kimeondoka jijini Dar es Salaam leo Alhamisi asubuhi kuelekea mkoani Dodoma tayari kushiriki michuano ya Ligi ya Vijana (Uhai Cup U-20) kwa timu za vijana za klabu zinazoshiriki Ligi Kuu.




« Previous Next »


User Detail Page

You can find user latest posts and related content on the page. Friends, comments for events / matches are also available on the page. Even you can find users who are same pleasure with current user.

#Travel, #SupportYourTeam, #AllAboutSports