Azam FC's user profile page. Match highlights, posts and more on site!“” Report User |
"Vijana wamesikitika na wasikate tamaa, watuombee dua, watusapoti tutapambana kwa ajili yao na kwa ajili ya timu yetu na nchi yetu, mpira umeanza sehemu ya kwanza, tuseme kama kipindi cha kwanza kimeanza lakini tutahakikisha kipindi cha pili tunapambana kwao kwa hali na mali ili tuweze kurudi na ushindi," alisema Kocha Msaidizi wa Azam FC, Idd Nassor 'Cheche', akiwaambia mashabiki wa timu hiyo. #TimuBoraBidhaaBora #AzamFC #TriangleUnited #CAFConfederationCup
Kikosi cha Azam FC kimerejea leo mchana jijini Dar es Salaam kikitokea mkoani Mbeya, kikiwa safi kabisa baada ya jana kuichapa Mbeya City bao 1-0 lililofungwa na beki Yakubu Mohammed. #WeAreAzamFC #TimuBoraBidhaaBora #AfricanFrutiImenogaFresh #UhaiDrinkingWater #TradegentsTanzaniaLimited
KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, imefanya kweli mkoani Mbeya baada ya kuichapa Mbeya City bao 1-0, mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) uliofanyika Uwanja wa Sokoine, Mbeya leo jumapili. Ushindi huo unaifanya Azam FC kufikisha jumla ya pointi 66 kwenye msimamo wa ligi ikiwa nafasi ya pili ikizidiwa pointi nane na kinara Yanga aliyekuwa nazo 74, Simba iliyocheza mechi 22 ni ya tatu ikijikusanyia 57. Beki wa Azam FC, Yakubu Mohammed, aliyeonekana kucheza vema kwenye eneo la beki ya kati sambamba na beki chipukizi kutoka Azam Academy, Lusajo Mwaikenda, ndiye aliyeipatia bao pekee timu hiyo dakika ya 45 akimalizia krosi iliyopigwa na kiungo, Mudathir Yahya, kufuatia mpira wa kona alioanzishiwa na Bruce Kangwa. #WeAreAzamFC #TimuBoraBidhaaBora #AfricanFrutiImenogaFresh #UhaiDrinkingWater #TradegentsTanzaniaLimited
#TPLRound24 KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, imeendeleza wimbi la ushindi kwenye mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) baada ya kuichapa Biashara United mabao 2-1. Mabao ya Azam FC, yamefungwa na kiungo Salum Abubakar 'Sure Boy' (46') kwa kichwa na Ramadhan Singano 'Messi' (62'), huku bao la kufuatia machozi la Biashara likiwekwa kimiani na Daniel Manyenye (2'). #TimuBoraBidhaaBora #AfricanFrutiImenogaFresh #UhaiDrinkingWater #TradegentsTanzaniaLimited
WAKATI zikiwa zimesalia siku mbili kabla ya Azam FC kumenyana na Biashara United, kikosi hicho kimejinasibu kuendelea kupata matokeo mazuri ili kufikia malengo yake. Mabingwa hao wa makombe mawili msimu huu baada ya kufanikiwa kutetea Kombe la Kagame na Mapinduzi Cup, wamekuwa kwenye mwenendo mzuri msimu huu hadi sasa ikishika nafasi ya pili kwenye za Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) ikiwa na pointi 44. Akizungumza na mtandao rasmi wa klabu www.azamfc.co.tz Nahodha wa Azam FC, Agrey Moris, amesema kuwa wanajua mchezo utakuwa mgumu lakini watajipanga vema kuweza kupata matokeo. “Biashara ni timu nzuri ukiangalia wamepata kocha mpya kwa vyovyote timu inayopata kocha mpya wachezaji wanakuwa wanajitolea mara mbili zaidi ya mwanzo ila kama sisi Azam siku zote tunajipanga kuhakikisha tunapata matokeo kwenye michezo yetu. “Kwa sababu hii ni ligi ni safari ndefu bila kushinda mechi inayokuja mbele huwezi ukafikia lengo, tumejipanga vizuri wachezaji wote wako vizuri tutahakikisha tunapata matokeo kwenye mchezo huo,” alisema mchezaji huyo wa muda mrefu wa Azam FC. Kihistoria timu hizo zimekutana mara moja tu kwenye ligi, tokea Biashara ipande kucheza Ligi Kuu msimu huu, ambapo mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Karume, mjini Musoma uliisha kwa suluhu. #TimuBoraBidhaaBora #AfricanFrutiImenogaFresh #UhaiDrinkingWater #TradegentsTanzaniaLimited