Content removal request!


Undani wa shangilia ya Messi vs Ruvu Shooting; Amtaja mwanaye

MASHABIKI wengi wa soka wamekuwa wakiwa na maswali mengi kuhusu staili ya ushangiliaji ya winga Ramadhan Singano ‘Messi’, aliyofanya jana Alhamisi mara baada ya kufunga bao dhidi ya Ruvu Shooting. Singano akizungumza na mtandao rasmi wa klabu www.azamfc.co.tz amesema kuwa ameshangilia bao kwa staili hiyo akimshukuru Mwenyezi Mungu baada ya kumjalia mke wake kupata mtoto wa kiume mwanzoni mwa wiki hii, akiwa ni mtoto wake wa kwanza kwenye maisha yake. “Staili yangu ni kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kumjalia mke wangu kunipa mtoto wa kiume, shangilia ile ilikuwa inamaanisha herufi ya ‘Y’ jina la baba yangu Yahya na mtoto wangu nikimpa jina la Yahya Ramdhan Singano,” alisema winga wa Azam FC, Ramadhan Singano 'Messi'. #TimuBoraBidhaaBora #AfricanFrutiImenogaFresh