Content removal request!


TPL ROUND 14 | Azam FC 2-1 Ruvu Shooting | Match Highlights

KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, imefanya kweli baada ya kuinyuka mabao 2-1 Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) uliomalizika kwenye Uwanja wa Azam Complex leo Alhamisi usiku. Ushindi huo unaihakikishia Azam FC nafasi ya kuendelea kubakia kileleni mwa msimamo wa ligi ikifikisha pointi 33 baada ya kushinda mechi 10 na sare tatu ikiwa haijapoteza mchezo hata mmoja.