BAADA ya jana kucheza mechi yake ya kwanza Azam FC akitokea kwenye majeruhi, mshambuliaji Donald Ngoma, ameonesha kufurahishwa sana huku akiwaahidi makubwa mashabiki wa timu hiyo. Azam FC iliyokuwa ikicheza na Lipuli jana usiku na kutoka suluhu, ilishuhudiwa Ngoma akiingia dakika ya 62 kuchukua nafasi ya kiungo mkabaji Mudathir Yahya, mchezo huo pia ukiwa ni wa kwanza kwake tokea asajiliwe na timu hiyo msimu huu akitokea Yanga. Licha ya kutoka kwenye majeraha ya takribani mwaka mmoja, Ngoma alionekana kuanza vema jana mechi yake ya kwanza akicheza kwa kujituma na kupambana na mabeki wa Lipuli huku akipata nafasi muhimu mbili za kufunga moja ikiwa ni ile ya kuangushwa katika eneo la hatari na kipa.
KLABU ya Azam FC imeanza vema kuwania ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania (VPL) msimu 2020/2021 baada ya kuichapa Polisi Tanzania bao 1-0 kwenye mchezo wa kwanza. Bao pekee la Azam FC limewekwa kambani na mshambuliaji Obrey Chirwa, dakika ya 44 akiunganisha krosi safi ya mshambuliaji mpya, Prince Dube. #WeAreAzamFC #TimuBoraBidhaaBora #SARAFU #AzamUkwaju #AzamUbuyu #AzamStrawberry #UhaiDrinkingWater
#ObreyChirwa #IddNado #AzamFC #SingidaUnited Azam FC imeandika rekodi ya kwanza baada ya kupata ushindi mnono wa kihistoria kwenye mechi za mashindano, ikiichapa Singida United mabao 7-0, ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL). Mabao ya Azam FC yalifungwa na Obrey Chirwa akifunga manne, Idd Seleman 'Nado', akifunga mawili huku jingine wakijifunga wenyewe Singida United. #WeAreAzamFC #TimuBoraBidhaaBora
KLABU ya Azam FC imeendelea pale ilipoishia kwenye mechi za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) baada ya kuichapa Mbaoa mabao 2-0 jana Jumapili usiku. Mabao ya Azam FC yalifungwa na washambuliaji Richard Djodi na Shaaban Chilunda. #WeAreAzamFC #TimuBoraBidhaaBora
HIGHLIGHTS | AZAM FC 2-2 JKT TANZANIA | 2019/2020 SEASON
Kikosi cha Azam FC kimeendeleza wimbi la ushindi ugenini kwenye mechi za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) kwa kupata ushindi mnono wa mabao 5-0 dhidi ya Alliance. Mabao matatu ya Obrey Chirwa (hat-trick) na mawili ya Shaaban Chilunda, yalitosha kabisa kuihakikishia ushindi mwingine Azam FC mkoani Mwanza, ikifanikiwa kuvuna pointi zote sita. #ObreyChirwa #ShaabanChilunda #WeAreAzamFC #TimuBoraBidhaaBora