Azam FC's user profile page. Match highlights, posts and more on site!“” Report User |
KIKOSI cha timu ya vijana ya Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Azam FC U-20, kimeondoka jijini Dar es Salaam leo Alhamisi asubuhi kuelekea mkoani Dodoma tayari kushiriki michuano ya Ligi ya Vijana (Uhai Cup U-20) kwa timu za vijana za klabu zinazoshiriki Ligi Kuu.
KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, imefanya kweli baada ya kuidungua Mwadui bao 1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) uliomalizika Uwanja wa Azam Complex usiku huu. Ushindi huo unaifanya Azam FC kusogea hadi nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ikifikisha jumla ya pointi 41 na kuishusha Yanga yenye mechi mbili mkononi hadi nafasi ya nne ikibakiwa na pointi zao 40 huku Simba ikiwa kileleni kwa pointi 46. Bao pekee la Azam FC limewekwa kimiani na mshambuliaji Yahya Zayd, dakika ya tano akitumia uzembe wa kipa wa Mwadui, Anold Massawe, aliyepiga mpira vibaya na kumpasia mguuni mfungaji wakati akiwa kwenye harakati za kuupiga mbele mpira aliorudishiwa na beki wake, Idd Mfaume.
KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, imeendeleza wimbi la ushindi kwenye Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) baada ya kuichapa Njombe Mji bao 1-0, mchezo uliofanyika Uwanja wa Sabasaba, mkoani Njombe jioni ya leo. Alikuwa ni Nahodha Msaidizi wa Azam FC, Agrey Moris aliyekuwa nahodha wa mchezo wa leo, akiihakikishia ushindi timu hiyo kwa bao safi la mkwaju wa penalti dakika ya 60 baada ya Enock Atta kufanyiwa madhambi kwenye eneo la hatari.