Content removal request!


Kagera vs Azam FC Post Match Press | Azam FC yajipanga kuendelea na moto TPL

BENCHI la ufundi la Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, limejipanga vilivyo kuwajenga wachezaji kisaikolojia na kisawasawa ili kuendelea na rekodi nzuri waliyoanza katika Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) msimu huu. Azam FC iliyoichapa Kagera Sugar leo bao 1-0 lililofungwa na Donald Ngoma, ipo kileleni kwa takribani wiki nne sasa ikifikisha jumla ya pointi 30 baada ya ushindi wa mechi tisa na sare tatu huku ikiwa haijapoteza mchezo hata mmoja. #AzamFCUnbeaten #AzamFCPopoteInakanyaga