WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwankyembe, leo alifanya ziara ya kutembelea Makao Makuu ya Azam FC ‘Azam Complex’ na kukiri kuwa timu hiyo ni kiwanda cha soka nchini. Ziara hiyo ya Mwakyembe ilikuwa ni maalumu kwa ajili ya kuangalia Azam FC ilipofikia kwenye uboreshaji wa uwanja huo ikiwa ni maandalizi ya kuelekea fainali za Mataifa ya Afrika kwa Vijana chini ya umri wa miaka 17 (AFCON U-17) zitakazofanyika nchini mwakani. Uwanja wa Azam Complex ni miongoni mwa viwanja vitatu nchini vilivyoteuliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kwa kushirikiana na la hapa nchini (TFF), vingine viwili vikiwa ni Uwanja wa Taifa na ule wa Uhuru. Kigogo huyo aliambatana na Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo Taifa (BMT), Alex Nkeyenge na Mkurugenzi wa Mashindano TFF, Salum Madadi, ambao walikaribishwa na wenyeji wao akiwemo Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Wakurugenzi, Nassor Idrissa ‘Father’, Makamu Mwenyekiti Omary Kuwe, Meneja wa timu, Philllip Alando. Akitoa neno kwenye ziara hiyo, Waziri Mwakyembe, aliupongeza uongozi wa Azam FC kwa kazi kubwa waliyofanya kwenye kuboresha uwanja huo kwa ajili ya fainali hizo ambazo zitafanyika kwa mara ya kwanza nchini. “Kwa kweli ni mara yangu ya kwanza kutembelea Azam Complex na nimejiridhisha mwenyewe kwamba hiki ni kiwanda cha soka, kiwanda cha michezo kuna kila kitu hapa na tukifikia hatua ambayo pengine timu zetu zenye sura ya Kitaifa hata zikawa tatu, nne, tano zikawa na mfumo ulioko hapa Azam Complex tayari sisi Tanzania tumeshakuwa nchi ya soka. “Na nadhani tutaanza kuuza wachezaji wengi sana duniani ambao pia watachangia sana katika pato la Taifa maana wenzetu wengi kama nchi ya Brazil inaendeshwa na pesa kama hiyo, Azam hongereni sana mmefanya kazi kubwa sana,” alisema.
KLABU ya Azam FC imeanza vema kuwania ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania (VPL) msimu 2020/2021 baada ya kuichapa Polisi Tanzania bao 1-0 kwenye mchezo wa kwanza. Bao pekee la Azam FC limewekwa kambani na mshambuliaji Obrey Chirwa, dakika ya 44 akiunganisha krosi safi ya mshambuliaji mpya, Prince Dube. #WeAreAzamFC #TimuBoraBidhaaBora #SARAFU #AzamUkwaju #AzamUbuyu #AzamStrawberry #UhaiDrinkingWater
#ObreyChirwa #IddNado #AzamFC #SingidaUnited Azam FC imeandika rekodi ya kwanza baada ya kupata ushindi mnono wa kihistoria kwenye mechi za mashindano, ikiichapa Singida United mabao 7-0, ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL). Mabao ya Azam FC yalifungwa na Obrey Chirwa akifunga manne, Idd Seleman 'Nado', akifunga mawili huku jingine wakijifunga wenyewe Singida United. #WeAreAzamFC #TimuBoraBidhaaBora
KLABU ya Azam FC imeendelea pale ilipoishia kwenye mechi za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) baada ya kuichapa Mbaoa mabao 2-0 jana Jumapili usiku. Mabao ya Azam FC yalifungwa na washambuliaji Richard Djodi na Shaaban Chilunda. #WeAreAzamFC #TimuBoraBidhaaBora
HIGHLIGHTS | AZAM FC 2-2 JKT TANZANIA | 2019/2020 SEASON
Kikosi cha Azam FC kimeendeleza wimbi la ushindi ugenini kwenye mechi za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) kwa kupata ushindi mnono wa mabao 5-0 dhidi ya Alliance. Mabao matatu ya Obrey Chirwa (hat-trick) na mawili ya Shaaban Chilunda, yalitosha kabisa kuihakikishia ushindi mwingine Azam FC mkoani Mwanza, ikifanikiwa kuvuna pointi zote sita. #ObreyChirwa #ShaabanChilunda #WeAreAzamFC #TimuBoraBidhaaBora