Azam FC, imelazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Alliance katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) uliofanyika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam. Ilibidi Azam FC iweze kusubiri hadi dakika ya 79 kuweza kupata bao la uongozi, lililofungwa na Joseph Mahundi, aliyeingia dakika ya 76, kuchukua nafasi ya Ramadhan Singano, na alifunga bao hilo kiustadi akiunganisha krosi ya Chirwa. Dakika ya 90 Alliance ilisawazisha kupitia kwa Dickson Ambundo, akimalizia mpira uliogonga mwamba kufuatia mpira wa adhabu ndogo uliopigwa na Israel Patrick. Azam walionekana kulalamikia bao hilo wakidai kuwa beki wao Agrey Moris alisukumwa kabla ya kufungwa lakini, mwamuzi Abubakar Mturo (Mtwara) na Msaidizi namba moja, Mohamed Mkono (Tanga), waliamuru kuwa bao halali.
Azam FC, imelazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Alliance katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) uliofanyika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam. Ilibidi Azam FC iweze kusubiri hadi dakika ya 79 kuweza kupata bao la uongozi, lililofungwa na Joseph Mahundi, aliyeingia dakika ya 76, kuchukua nafasi ya Ramadhan Singano, na alifunga bao hilo kiustadi akiunganisha krosi ya Chirwa. Dakika ya 90 Alliance ilisawazisha kupitia kwa Dickson Ambundo, akimalizia mpira uliogonga mwamba kufuatia mpira wa adhabu ndogo uliopigwa na Israel Patrick. Azam walionekana kulalamikia bao hilo wakidai kuwa beki wao Agrey Moris alisukumwa kabla ya kufungwa lakini, mwamuzi Abubakar Mturo (Mtwara) na Msaidizi namba moja, Mohamed Mkono (Tanga), waliamuru kuwa bao halali. Mchezo huo ulikuwa na kasi sana, Azam FC ikianza kwa mashambulizi makali langoni mwa Alliance, ambapo dakika ya kwanza Obrey Chirwa, alikosa bao la wazi baada ya kuupiga vibaya mpira akiwa anatazamana na lango ndani ya eneo la hatari, akipokea pasi ya Donald Ngoma. Mabingwa hao waliweza kupata ugumu kuipenya safu ya ulinzi ya Alliance, kutokana na timu hiyo kusimama wengi kujilinda nyuma ya mpira wakati Azam FC ikishambulia. Mara baada ya mchezo huo kumalizika, kipa wa Azam FC, Razak Abalora, alioneshwa kadi nyekundu kufuatia kadi ya pili ya njano iliyosababishwa na lugha ya kutoridhishwa na maamuzi aliyoitoa kwa mwamuzi huyo. Sare hiyo inaifanya Azam FC kufikisha jumla ya pointi 48 katika nafasi ya pili kwenye msimamo ikiwa na mchezo mmoja mkononi, ikizidiwa pointi saba na kinara Yanga aliyefikisha 55 kufuatia suluhu yake ya jana dhidi ya Singida United.
‘Wana-kuchele’ Ndanda SC leo wamevunja mwiko wa kutopata ushindi mbele ya Mnyama mkali Simba baada ya kuilazimisha suluhu katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa kwenye dimba la Nangwanda Sijaona, mjini Mtwara. Katika mchezo huo uliokuwa wa upande mmoja, wenyeji Ndanda waliingia na mbinu ya kuzuia zaidi na kuwaacha Simba wacheze mpira hasa kwenye eneo ambalo halikuwa na hatari yoyote. Mabingwa watetezi, Simba licha ya kuwaanzisha washambuliaji watatu machachari, Emmanuel Okwi, Meddie Kagere na John Bocco, ilishindwa kutengeza nafasi za wazi kutokana na washambuliaji hao kudhibitiwa vilivyo na mabeki wa Ndanda. Hadi mwisho wa mchezo, Simba ilikuwa imepiga jumla ya mashuti 17 ambapo kati ya hayo ni mashuti matatu pekee ndiyo yaliyolenga lango, huku Ndanda wakiwa wamepiga jumla ya mashuti matatu na moja pekee likiwa ndilo limenga lango. Hii ni mara ya kwanza Ndanda FC inakataa kufungwa na Simba, tangu ipande Ligi Kuu Tanzania Bara mwaka 2013. Baada ya mchezo huo, Nahodha wa Simba John Bocco amesema licha ya matokeo hayo kutowafurahisha, wanayasahau na kuanza kujipanga kwaajili ya mchezo ulio mbele yao huku kocha wa Ndanda Malale Hamsini akisema aliamua kutumia mbinu hiyo kutokana na ukubwa wa timu ya Simba. Matokeo hayo yanaiweka Simba katika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 7, huku Ndanda wakifikisha pointi 4 katika nafasi ya 12.
Ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Ndanda SC na Mwadui FC inayopigwa dimba la Nangwanda Sijaona mjini Mtwara, ambapo hadi kipindi cha kwanza kinamalizika, Ndanda walikuwa mbele kwa mabao 3-0. Ndanda FC ambayo inapigania kutoshuka daraja, imeanza kwa kasi na kujipatia magoli matatu ndani ya kipindi cha kwanza kupitia kwa Jacob Massawe dakika ya 3, Mrisho Ngassa dakika ya 5 na Tibar John dakika ya 40. Mabao hayo yamedumu hadi mwisho wa mchezo, na kuifanya Ndanda FC kuibuka na ushindi wa mabao 3-0.
Timu ya Ndanda FC wamekubali kupokea kichapo cha mabao 3-1 katika uwanja wake wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara ukiwa ni mwendelezo wa harakati za ‘mpapaso’ wa wanamgambo wa timu ya Ruvu kwa kila timu ambayo watakutana nayo. Msemaji wa klabu ya Ruvu Shooting Massau Bwire amesema ‘wataipapasa’ kila timu itakayokuwa mbele yao.
Ni mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara uliopigwa katika dimba la Nangwanda Sijaona Mtwara ambapo Simba imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 yote yakifungwa na Nahodha wake John Bocco
Msanii kutoka lebo ya WCB Wasafi,Harmonize leo alikuwepo uwanjani Nangwanda mjini Mtwara, kuishabikia timu ya nyumbani kwao Ndanda Fc iliyokua ikikipiga na Simba Sc. Harmonize aliyeongozana na mpenzi wake Sarah alikua akipiga ngoma kushabikia kikosi chao. SUBSCRIBE Katika YouTube Chanel Yetu Kuendelea Kupata Habari Mpya za Michezo Kila Zinavyotufikia https://www.youtube.com/channel/UC5fuHg4PI1GAn_U4S5cAOjQ?view_as=subscriber https://www.youtube.com/channel/UC5fuHg4PI1GAn_U4S5cAOjQ?view_as=subscriber https://www.youtube.com/channel/UC5fuHg4PI1GAn_U4S5cAOjQ?view_as=subscriber https://www.youtube.com/channel/UC5fuHg4PI1GAn_U4S5cAOjQ?view_as=subscriber https://www.youtube.com/channel/UC5fuHg4PI1GAn_U4S5cAOjQ?view_as=subscriber https://www.youtube.com/channel/UC5fuHg4PI1GAn_U4S5cAOjQ?view_as=subscriber
Mkali wa bongo fleva kutoka WCB, Harmonize ambaye ni mwenyeji wa mkoa wa Mtwara, naye alikuwepo katika dimba la Nangwanda Sijaona, akiongoza timu ya mashabiki wa Ndanda FC. FT: Ndanda FC 0-2 Simba SC.