Content removal request!


AZAM FC 1-1 ALLIANCE FC: HIGHLIGHTS & INTERVIEWS (TPL - 6/2/2019)

Azam FC, imelazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Alliance katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) uliofanyika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam. Ilibidi Azam FC iweze kusubiri hadi dakika ya 79 kuweza kupata bao la uongozi, lililofungwa na Joseph Mahundi, aliyeingia dakika ya 76, kuchukua nafasi ya Ramadhan Singano, na alifunga bao hilo kiustadi akiunganisha krosi ya Chirwa. Dakika ya 90 Alliance ilisawazisha kupitia kwa Dickson Ambundo, akimalizia mpira uliogonga mwamba kufuatia mpira wa adhabu ndogo uliopigwa na Israel Patrick. Azam walionekana kulalamikia bao hilo wakidai kuwa beki wao Agrey Moris alisukumwa kabla ya kufungwa lakini, mwamuzi Abubakar Mturo (Mtwara) na Msaidizi namba moja, Mohamed Mkono (Tanga), waliamuru kuwa bao halali. Mchezo huo ulikuwa na kasi sana, Azam FC ikianza kwa mashambulizi makali langoni mwa Alliance, ambapo dakika ya kwanza Obrey Chirwa, alikosa bao la wazi baada ya kuupiga vibaya mpira akiwa anatazamana na lango ndani ya eneo la hatari, akipokea pasi ya Donald Ngoma. Mabingwa hao waliweza kupata ugumu kuipenya safu ya ulinzi ya Alliance, kutokana na timu hiyo kusimama wengi kujilinda nyuma ya mpira wakati Azam FC ikishambulia. Mara baada ya mchezo huo kumalizika, kipa wa Azam FC, Razak Abalora, alioneshwa kadi nyekundu kufuatia kadi ya pili ya njano iliyosababishwa na lugha ya kutoridhishwa na maamuzi aliyoitoa kwa mwamuzi huyo. Sare hiyo inaifanya Azam FC kufikisha jumla ya pointi 48 katika nafasi ya pili kwenye msimamo ikiwa na mchezo mmoja mkononi, ikizidiwa pointi saba na kinara Yanga aliyefikisha 55 kufuatia suluhu yake ya jana dhidi ya Singida United.