‘Wana-kuchele’ Ndanda SC leo wamevunja mwiko wa kutopata ushindi mbele ya Mnyama mkali Simba baada ya kuilazimisha suluhu katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa kwenye dimba la Nangwanda Sijaona, mjini Mtwara. Katika mchezo huo uliokuwa wa upande mmoja, wenyeji Ndanda waliingia na mbinu ya kuzuia zaidi na kuwaacha Simba wacheze mpira hasa kwenye eneo ambalo halikuwa na hatari yoyote. Mabingwa watetezi, Simba licha ya kuwaanzisha washambuliaji watatu machachari, Emmanuel Okwi, Meddie Kagere na John Bocco, ilishindwa kutengeza nafasi za wazi kutokana na washambuliaji hao kudhibitiwa vilivyo na mabeki wa Ndanda. Hadi mwisho wa mchezo, Simba ilikuwa imepiga jumla ya mashuti 17 ambapo kati ya hayo ni mashuti matatu pekee ndiyo yaliyolenga lango, huku Ndanda wakiwa wamepiga jumla ya mashuti matatu na moja pekee likiwa ndilo limenga lango. Hii ni mara ya kwanza Ndanda FC inakataa kufungwa na Simba, tangu ipande Ligi Kuu Tanzania Bara mwaka 2013. Baada ya mchezo huo, Nahodha wa Simba John Bocco amesema licha ya matokeo hayo kutowafurahisha, wanayasahau na kuanza kujipanga kwaajili ya mchezo ulio mbele yao huku kocha wa Ndanda Malale Hamsini akisema aliamua kutumia mbinu hiyo kutokana na ukubwa wa timu ya Simba. Matokeo hayo yanaiweka Simba katika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 7, huku Ndanda wakifikisha pointi 4 katika nafasi ya 12.
#NBCPL: Tazama magoli yote matano yaliyofungwa kwenye mchezo wa NBC Premier League kati TRA United dhidi ya Azam FC. FT: TRA United 4-1 Azam FC Magoli ya TRA United yamefungwa na Ally Ng'azi, Ammy Mapaka na Ramadhan Salum 'Chobwedo' Goli la Azam FC limefungwa na Jephte Kitambala Bola. #NBCPremierLeague #LigiKuuYaNBC #NBCPL #NBCPLUpdates #ImenogaZaidi #TRAUnitedvsAzamFC #TRAUnited #AzamFC #TRAUnitedAzamFC
KARIAKOO DERBY | Imepigwa dabi moja ya maana sana kwenye Dimba la Amaan, Zanzibar, Yanga na Simba wakimaliza dakika 90 bila bao, lakini burudani za kutosha. Hii ni mechi ya Ligi Kuu ya NBC Tanzania
Yanga SC imeichakaza JKT Tanzania mabao 5-0 katika mchezo wa ligi kuu ya NBC uliopigwa leo kwenye Dimba la KMC Complex, Dar es Salaam. Wafungaji wa magoli haya ni Mohamed Hussein Zimbwe Jr,, Aurellio Depu, Mudathir Yahya, Prince Dube na Shekhan Ibrahim.
Ni mechi ya kirafiki ya kalenda ya FIFA iliyopigwa kwenye Dimba la Al Salaam, Cairo nchini Misri, na timu ya taifa ya Tanzania #TaifaStars kuchwa 4-3 na Kuwait. Magoli ya Tanzania yamefungwa na M’mombwa 6’, 87’, na Taryin Allarakhia 34’ huku ya Kuwait yakitoka kwa Daham 46’, 52’ Nasser 63’ na Hamdan 69’
KMC vs SINGIDA BS: Kocha Marcio Maximo wa KMC, amesema mataifa ya Argentina na Brazil ni wapinzani ndani ya uwanja, ...
KARIAKOO DEEBY | Fahamu ukweli kuhusu matukio yote yaliyozua utata kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii kati ya Yanga na Simba uliopigwa Septemba 16, 2025. Moja kati ya matukio yaliyozua gumzo ni goli pekee walilofunga Yanga na kuamua mshindi wa Ngao ya Jamii 2025. Osman Kazi na jopo lake wanamaliza utata kwa kutumia sheria na kanuni za soka
KUTOKA CAIRO MISRI: " ....msimu huu tunahitaji kuwapiku Yanga" Baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Wadi Degla FC inayoshiriki ligi kuu ya nchini humo, Kocha wa Simba, Fadlu davids anaeleza baadhi ya mambo ambayo ameridhika nayo, na maeneo ambayo bado ana kazi ya kufanya.... Kuhusu kikosi chake, Kocha Fadlu anasema bado wanahitaji angalau mchezaji mmoja mwenye kitu cha ziada (X-Factor) atakayewaongezea kitu hasa kwenye michuano ya kimataifa pamoja na mbio za ubingwa wa #NBCPremierLeague msimu ujao wakilenga kuwa juu ya Yanga ... Fadlu anasema anaamini mdhamini wao upande wa jezi, 'Jayruty', atalimaliza hilo.... Naye mfungaji wa moja kati ya magoli mawili ya Simba, Kibu Denis anazungumza machache kuhusu maendeleo ya kambi nchini Misri.... Patrick Nyembera anakuja na taarifa kamli kuhusu mchezo huo... #SimbaSC #SimbaEgypt #SimbaPreSeason
Yanga SC imepata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Rayon Sports, katika mchezo wa kirafiki uliopigwa kwenye Dimba la Amahoro, jijini Kigali, Rwanda. Mchezo huo uliokuwa hitimisho la Siku ya Rayon Sports #RayonSportsDay , umeshuhudia wenyeji wakitangulia kwa goli la kujifunga kupitia kwa Aziz Andambwile. Yanga walicharuka na kupiga mabao matatu kupitia kwa Andy Boyeli, Pacome Zouzoua, na Bakari Mwamnyeto.