MAGOLI: COASTAL UNION 1-1 MBEYA CITY  (TPL - 09/12/2018)
MAGOLI: COASTAL UNION 1-1 MBEYA CITY (TPL - 09/12/2018)

Wagosi wa Kaya Coastal Union wakiwa na Alikiba aliyecheza kwa dakika 64, wamebanwa nyumbani na kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa kwenye Dimba la Mkwakwani Jijini Tanga. Coastal ndiyo waliotangulia kupata bao dakika ya 5 kupitia kwa Ayoub Lyanga aliyemalizia kwa kichwa kona iliyopigwa na Athuman Idd ‘Chuji’ ikitokana na jaribio la Alikiba. Mbeya City walipata bao la kusawazisha dakika ya 50 baada ya beki wa Coastal Union Bakari Mwamnyeto kujifunga akiwa katika jaribio la kuokoa. Haya hapa mabao.



KIPYENGA CHA MWISHO: "Goli moja la Simba dhidi ya JKT Tanzania halikuwa halali" (08/11/2018)
KIPYENGA CHA MWISHO: "Goli moja la Simba dhidi ya JKT Tanzania halikuwa halali" (08/11/2018)

Kwa mujibu wa kipindi hiki cha terehe 08/11/2018, bao la pili alilofunga Meddie Kagere kwenye mchezo kati ya JKT Tanzania vs Simba SC uliopigwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga Jumamosi ya Novemba 2, 2018, halikuwa bao halali kwa kuwa mfungaji alikuwa ameotea kabla ya kufunga. Pamoja na matukio mengine yaliyojiri kwenye mchezo huo, pia palikuwa na matukio mawili ya wachezaji wa JKT kudai penati wakidai wachezaji wa Simba Mohamed Hussein na Erasto Nyoni kwa nyakati tofauti, walishika mpira ndani ya eneo la hatari hadi kusababisha mchezaji wa JKT Ahmed Shiboli kutolewa nje kwa kadi nyekundu. Mbali na mchezo huo, kipindi hiki kimechambua mechi kdhaa za raundi ya 13 ya Ligi Kuu Tanzania Bara ukiwemo mchezo wa Yanga vs Ndanda SC na ule wa Kagera Sugar vs Azam FC. Tukio kubwa katika mchezo wa Kagera Sugar na Azam FC ni mchezaji wa Azam FC Donald Ngoma kupewa kadi nyekundu, kadi ambayo wengi hawakuelewa sababu za adhabu hiyo kumkumba. Waamuzi wawili wastaafu ambao ni magwiji, Osman Kazi na Omary Abdulkadir wamechambua matukio yote na kuonesha ni wapi waamuzi walikosea na wapi waamuzi walipatia, na nini walipaswa kufanya. Kipyenga cha Mwisho ni kila Alhamis saa 3:30 usiku Azam Sports 2.



JKT TANZANIA 0-2 SIMBA SC; HIGHLIGHTS & INTERVIEWS (TPL 03/11/2018)
JKT TANZANIA 0-2 SIMBA SC; HIGHLIGHTS & INTERVIEWS (TPL 03/11/2018)

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara wamepata ushindi wa mabao 2-0 wakiwa ugenini dhidi ya JKT Tanzania, mchezo ukipigwa kwenye Dimba la Mkwakwani mkoani Tanga. Mabao yote ya Simba yamefungwa na mshambuliaji wao Meddie Kegere dakika ya 12 na 38, kazi nzuri ikifanywa na Emmanuel Okwi. Mshambuliaji wa JKT Tanzania Ally Ahmed Shiboli ambaye aliingia kutokea benchi, alikumbana na rungu la mwamuzi Mbaraka Rashid baada ya kuonesha kitendo cha utovu wa nidhamu dhidi ya mwamuzi huyo. Tukio hilo limetokea dakika ya 88 wakati wachezaji wa JKT Tanzania wakidai kunyimwa penati baada ya mpira kumgonga mkononi beki wa Simba, Erasto Nyoni. Mchezo huu pia ulikumbwa na tafran dakika za mwisho. Baada ya mchezo, upande wa JKT ulikataa kufanya mahojiano, huku upande wa Simba akizungumza nahodha wao John Bocco.



Alichosema KOCHA SIMBA, Kotei, Chama, Mkwakwani Tanga
Alichosema KOCHA SIMBA, Kotei, Chama, Mkwakwani Tanga

Mambo mawili yaliyofungwa na Meddie Kagere katika dakika za 11 na 38 kipindi cha kwanza yameiwezesha Simba kung'ara kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya JKT Tanzania. Katika mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa CCM Mkwakwani Tanga, Simba ilimuazisha kiungo wake Mghana, James Kotei ambaye alikuwa anatumikia adhabu kufuatia kumpiga Gadiel Michael katika mechi ya mwisho iliyowakutanisha watani wa jadi. Ushindi huo unaifanya Simba kuendelea kuikimbiza Azam FC iliyo na pointi 27 kileleni kwa kufikisha alama 26. Licha ya ushindi huo, Kocha Patrick Aussems ameulalamikia Uwanja wa Mkwakwani kuwa si rafiki kwa kuchezea na akiomba kama kuna uwezekano uweze kufanyiwa ukarabati. #JKTTanzania #SIMBASC #MeddieKagere



Kadi nyekundi kwa Ahmed Shiboli ilivyotokea; JKT Tanzania 0-2 Simba SC (TPL – 03/11/2018)
Kadi nyekundi kwa Ahmed Shiboli ilivyotokea; JKT Tanzania 0-2 Simba SC (TPL – 03/11/2018)

Mshambuliaji wa JKT Tanzania Ally Ahmed Shiboli ambaye aliingia kutokea benchi, alikumbana na rungu la mwamuzi Mbaraka Rashid baada ya kuonesha kitendo cha utovu wa nidhamu dhidi ya mwamuzi huyo. Tukio hilo limetokea dakika ya 88 wakati wachezaji wa JKT Tanzania wakidai kunyimwa penati baada ya mpira kumgonga mkononi beki wa Simba, Erasto Nyoni. Mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga umemalizika kwa Simba kupata ushindi wa mabao 2-0. Tazama ilivyokuwa.



JKT Tanzania 'yazipeleka' Simba na Yanga Mkwakwani Tanga
JKT Tanzania 'yazipeleka' Simba na Yanga Mkwakwani Tanga

Timu ya JKT Tanzania imeamua kutumia Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga kama uwanja wake wa nyumbani kwa mechi za Ligi Kuu Tanzania zitakazohusisha Simba na Yanga. Uamuzi huo unatokana na uwanja wake wa nyumbani inaotumia sasa wa Meja Jenerali Isamuhyo ulioko Mbweni Dar es Salaam, kutokuwa na uwezo wa kuhimili wingi wa mashabiki wa timu hizo mbili vigogo nchini Tanzania.



COASTAL UNION 1-0 MWADUI FC; HIGHLIGHTS & INTERVIEWS (TPL - 01/10/2018)
COASTAL UNION 1-0 MWADUI FC; HIGHLIGHTS & INTERVIEWS (TPL - 01/10/2018)

Wagosi wa Kaya Coastal Union wamepata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Mwadui FC katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa leo kwenye Dimba la Mkwakwani mkoani tanga. Bao pekee la Coastal limefungwa na Deogratius Anthony dakika ya 36. Tazama Highlights za mchezo wenyewe



Bao pekee la Coastal Union kwenye ushindi wa 1-0 dhidi ya Mwadui FC (TPL - 01/10/2018)
Bao pekee la Coastal Union kwenye ushindi wa 1-0 dhidi ya Mwadui FC (TPL - 01/10/2018)

Wagosi wa Kaya Coastal Union wamepata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Mwadui FC katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa leo kwenye Dimba la Mkwakwani mkoani tanga. Bao pekee la Coastal limefungwa na Deogratius Anthony dakika ya 36. Hivi ndivyo ilivyokuwa.




« Previous Next »


Popular Tags

#Kawhi Leonard  #Neymar  #Kevin Durant  #Tristan Thompson  #Miami Heat  #Lionel Messi  #Best Goalkeeper Saves  #Counter Attack Goals Football  #Goal Celebrations  #LeBron James  

Popular Users

#ochocinco  #THNRyanKennedy  #themichaelowen  #BizNasty2point0  #baseballpro  #SrBachchan  #realDonaldTrump  #CMPunk  #twitter  #itsBayleyWWE  #Drake  #serenawilliams  #TheCUTCH22