Goli pekee lililofungwa na kiungo Feisal Salum ‘Feitoto’ dakika ya 27, limeipa Yanga ushindi wa bao 1-0 dhidi ya JKT Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa leo kwenye Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga. Feisal amefunga goli hilo akimalizia pasi ya Gadiel Michael kutoka winga ya kushoto na kuwafanya mabingwa hao wa kihistoria wa ligi hiyo kuondoka na alama tatu muhimu zinazowafanya kujikita kileleni kwa kufikisha pointi 58 mbele ya Azam FC yenye pointi 48 na Simba yenye pointi 36. Matokeo haya pia yanawapoza machungu Yanga kutokana na matokeo ya michezo mitatu iliyopita ambayo hawakupata ushindi wakifungwa mchezo mmoja na kutoka sare michezo miwili.

Alichokisema Msemaji wa Ruvu Shooting Masau Bwire kuelekea mchezo wao wa leo dhidi ya Coastal Union. Mechi ni Februari 7, 2019 saa 10:00 jioni kwenye dimba la Mkwakwani mkoani LIVE #AzamSports2
Mabingwa wa kihistoria wa Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga SC ya Dar es Salaam, leo wameambulia pointi moja wakilazimisha sare ya bao 1-1 ugenini dhidi ya Coastal Union katika mchezo wa ligi hiyo uliopigwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga. Wenyeji Coastal Union ndiyo waliotangulia kupata bao dakika ya 30 kupitia kwa Haji Ugando aliyemalizia kwa kichwa krosi ya Ayoub Lyanga, huku Yanga wakisawazisha dakika ya 76 kupitia kwa Deus Kaseke akimalizia pasi ya Matheo Anthony. Katika mchezo huo Coastal Union walikumbana na pigo kwa mshambuliaji wake Issa Abushehe kutolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kumpiga teke kwa makusudi mchezaji wa Yanga na dakika moja baadaye Yanga wakasawazisha. Dakika ya 81, mshambuliaji wa Coastal Union Andrew Simchimba alianguka ndani ya eneo la hatari la Yanga na kudai penati lakini mwamuzi hakutoa penati na alimuonesha kadi ya njano akimaanisha kuwa Simchimba alijiangusha. Dakika ya 40 ya mchezo, beki wa Yanga Abdallah Haji Shaibu ‘Ninja’ alionekana kumpiga kiwiko mchezaji wa Coastal Union lakini mwamuzi hakuliona tukio hilo, na dakika ya 7 Yanga walitikisa nyavu za Coastal lakini mwamuzi aliamua kuwa ilikuwa ni off side. Kwa matokeo hayo Yanga inaendelea kukaa kileleni ikiwa na pointi 54, huku Coastal Union wakipanda kutoka nafasi ya 10 hadi ya 8.
Wagosi wa Kaya timu ya Coastal Union imepata ushindi wa mabao 2-0 katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) uliopigwa leo kwenye Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga. Mabao ya Coastal Union waliokuwa wenyeji wa mchezo yamefungwa na Andrew Simchimba dakika ya 49 akimalizia mpira wa kurusha na Issa Abushehe dakika ya 90’+1 akimalizia pasi ya Haji Ugando.

Ni baada ya mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa Jumapili ya Desemba 9, 2018 kwenye Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga na kumalika kwa sare ya bao 1-1.
Wagosi wa Kaya Coastal Union wakiwa na Alikiba aliyecheza kwa dakika 64, wamebanwa nyumbani na kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa kwenye Dimba la Mkwakwani Jijini Tanga. Coastal ndiyo waliotangulia kupata bao dakika ya 5 kupitia kwa Ayoub Lyanga aliyemalizia kwa kichwa kona iliyopigwa na Athuman Idd ‘Chuji’ ikitokana na jaribio la Alikiba. Mbeya City walipata bao la kusawazisha dakika ya 50 baada ya beki wa Coastal Union Bakari Mwamnyeto kujifunga akiwa katika jaribio la kuokoa.