HIGHLIGHTS & INTERVIEWS: LIPULI FC 1-0 ALLIANCE FC; (TPL - 19/09/2018)
HIGHLIGHTS & INTERVIEWS: LIPULI FC 1-0 ALLIANCE FC; (TPL - 19/09/2018)

Lipuli FC ya Iringa wameichapa Alliance kutoka Jijini Mwanza bao 1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa leo kwenye dimba la Samora mjini Iringa. Bao pekee la Lipuli limepatikana dakika ya 6 ya mchezo kupitia kwa Miraji Athuman kwa kichwa akiitumia vizuri kros kutoka upande wa kulia. Katika mchezo huo Lipuli walitawala zaidi kipindi cha kwanza kwa mashambulizi mfululizo, lakini Kipindi cha pili alliance waliamka na kuonesha dalili za kusawazisha, lakini haikuwa hivyo. Hata hivyo dakika ya 50, Alliance walifanikiwa kutikisa nyavu za Lipuli lakini mwamuzi akaamua kuwa mfungaji alikuwa off-side na hadi mwisho wa mchezo, Alliance wakaondoka na kipigo hicho cha bao 1-0, kikiwa ni kipigo cha tatu mfululizo. Tazama highlights za mchezo.



Mtibwa Sugar 2-1 Mbeya City: Walichozungumza makocha na wachezaji (TPL 01/09/2018)
Mtibwa Sugar 2-1 Mbeya City: Walichozungumza makocha na wachezaji (TPL 01/09/2018)

Timu ya Mtibwa Sugar ya mkoani Morogoro imeendeleza ushindi katika dimba lake la nyumbani la Manungu baada ya leo kuifunga Mbeya City mabao 2-1 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL). Mara baada ya mchezo huo, Azam TV imezungumza na makocha wa timu zote mbili Ramadhan Swanzurimo wa Mbeya City na Zuberi Katwila wa Mtibwa Sugar, wote wameeleza sababu za kitaalamu za matokeo hayo. Pia Azam TV imezungumza na baadhi ya wachezaji waliong’ara kwenye mchezo huo, Stamili Mbonde ambaye ni mfungaji wa bao la kwanza la Mtibwa, Ismail Aidan Mhesa ambaye ni mfungaji wa bao la pili la Mtibwa na Eric Kyaruzi ambaye ni mfungaji wa bao pekee la Mbeya City.



HIGHLIGHTS: COASTAL UNION 1-0 BIASHARA UNITED; (TPL 25/08/2018)
HIGHLIGHTS: COASTAL UNION 1-0 BIASHARA UNITED; (TPL 25/08/2018)

Timu ya Coastal Union ya Tanga imepata ushindi wa bao 1-0 kwenye mchezo wa raundi ya pili ya Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa leo kwenye Dimba la CCM Mkwakwani, Jijini Tanga. Bao pekee la Coastal Union kwenye mchezo huo limefungwa na Haji Ugando dakika ya 20 ya mchezo. Katika mchezo huo, Coastal walianza kwa kasi na kufanikiwa kutikisa nyavu dakika ya 4 lakini ilikuwa ni off side, na kisha kupata penati dakika ya 13 lakini Mkwaju wa Mtenje Juma ukapanguliwa na kipa wa Biashara United Balora Nasridine. Biashara United walionekana kumlalamikia mwamuzi wa pembani baada ya kukataa bao lao la dakika ya 45 kwa madai kuwa mfungaji alikuwa ameotea. Mara baada ya mchezo, manahodha wa pande zote mbili wamezungumza. Tazama highlights.



Azam FC ilivyoiondoa Yanga nafasi ya pili kwa kuichapa Mwadui bao 1-0 - March 8, 2018
Azam FC ilivyoiondoa Yanga nafasi ya pili kwa kuichapa Mwadui bao 1-0 - March 8, 2018

KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, imefanya kweli baada ya kuidungua Mwadui bao 1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) uliomalizika Uwanja wa Azam Complex usiku huu. Ushindi huo unaifanya Azam FC kusogea hadi nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ikifikisha jumla ya pointi 41 na kuishusha Yanga yenye mechi mbili mkononi hadi nafasi ya nne ikibakiwa na pointi zao 40 huku Simba ikiwa kileleni kwa pointi 46. Bao pekee la Azam FC limewekwa kimiani na mshambuliaji Yahya Zayd, dakika ya tano akitumia uzembe wa kipa wa Mwadui, Anold Massawe, aliyepiga mpira vibaya na kumpasia mguuni mfungaji wakati akiwa kwenye harakati za kuupiga mbele mpira aliorudishiwa na beki wake, Idd Mfaume.



VPL: MBEYA CITY VS STAND UNITED
VPL: MBEYA CITY VS STAND UNITED

Goli la Mbeya City lililokataliwa kutokana na mfungaji kuotea.



Emmanuel Okwi Mfungaji Bora Ligi Kuu
Emmanuel Okwi Mfungaji Bora Ligi Kuu

Mshambuliaji nyota wa Simba , Emmanuel Okwi amefunga bao 1 dhidi ya timu ya Simba kwenye Uwanja wa Taifa.



KOCHA AZAM FC: SIMBA HAWANA LOLOTE, WAMEBAHATISHA
KOCHA AZAM FC: SIMBA HAWANA LOLOTE, WAMEBAHATISHA

KOCHA AZAM FC: SIMBA HAWANA LOLOTE, WAMEBAHATISHA SIMBA SC imezidi kuwaacha mbali wapinzani katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Azam FC jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Hongera kwake mfungaji wa bao pekee la leo, mshambuliaji Mganda Emmanuel Arnold Okwi aliyefunga dakika ya 36 baada ya kutokea patashika kwenye lango la Azam FC kufuatia krosi ya beki Mghana, Asante Kwasi. Simba SC sasa inafikisha pointi 41 baada ya kucheza mechi 17, wakiwazidi kwa pointi saba, mabingwa watetezi, Yanga SC wenye pointi 34 katika nafasi ya pili na Azam FC wanabaki nafasi ya tatu kwa pointi zao 33. Subscribe muda huu www.youtube.com/user/uwazi1 Install #GlobalPublishersApp Android: http://bit.ly/2AAQe1d iOS: http://apple.co/2Assf4M Subscribe http://www.youtube.com/c/uwazi FACEBOOK: https://www.facebook.com/Globalpublis... TWITTER: https://twitter.com/GlobalHabari Visit https://globalpublishers.co.tz/, Subscribe http://www.youtube.com/c/uwazi1 Kupata video nyingine za aina hii, subscribe kwenye chanell yetu kwa kubofya… http://www.youtube.com/c/uwazi1 http://www.youtube.com/c/uwazi1 http://www.youtube.com/c/uwazi1 WEBSITE: https://globalpublishers.co.tz/ FACEBOOK: https://www.facebook.com/Globalpublis... TWITTER: https://twitter.com/GlobalHabari INSTAGRAM: https://www.instagram.com/globalpubli..



KOCHA SIMBA Afungukia Siri ya Ushindi Dhidi ya Azam
KOCHA SIMBA Afungukia Siri ya Ushindi Dhidi ya Azam

KOCHA SIMBA Afungukia Siri ya Ushindi Dhidi ya Azam SIMBA SC imezidi kuwaacha mbali wapinzani katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Azam FC jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Hongera kwake mfungaji wa bao pekee la leo, mshambuliaji Mganda Emmanuel Arnold Okwi aliyefunga dakika ya 36 baada ya kutokea patashika kwenye lango la Azam FC kufuatia krosi ya beki Mghana, Asante Kwasi. Simba SC sasa inafikisha pointi 41 baada ya kucheza mechi 17, wakiwazidi kwa pointi saba, mabingwa watetezi, Yanga SC wenye pointi 34 katika nafasi ya pili na Azam FC wanabaki nafasi ya tatu kwa pointi zao 33. Subscribe muda huu www.youtube.com/user/uwazi1 Install #GlobalPublishersApp Android: http://bit.ly/2AAQe1d iOS: http://apple.co/2Assf4M Subscribe http://www.youtube.com/c/uwazi FACEBOOK: https://www.facebook.com/Globalpublis... TWITTER: https://twitter.com/GlobalHabari Visit https://globalpublishers.co.tz/, Subscribe http://www.youtube.com/c/uwazi1 Kupata video nyingine za aina hii, subscribe kwenye chanell yetu kwa kubofya… http://www.youtube.com/c/uwazi1 http://www.youtube.com/c/uwazi1 http://www.youtube.com/c/uwazi1 WEBSITE: https://globalpublishers.co.tz/ FACEBOOK: https://www.facebook.com/Globalpublis... TWITTER: https://twitter.com/GlobalHabari INSTAGRAM: https://www.instagram.com/globalpubli..




« Previous Next »


Popular Tags

#Best Ball Controls  #Kyrie Irving  #Shaquille O'Neal  #Michael Jordan  #Counter Attack Goals Football  #Best Goals Ever  #Golden State Warriors  #Kevin Durant  #Gareth Bale  #Boston Celtics  

Popular Users

#katyperry  #JasonDufner  #MichelleDBeadle  #BellaTwins  #TimTebow  #billbarnwell  #TheChristinaKim  #nfl  #britneyspears  #normmacdonald  #Buccigross  #Cristiano  #hunterpence  #BeingSalmanKhan