Timu ya Coastal Union ya Tanga imepata ushindi wa bao 1-0 kwenye mchezo wa raundi ya pili ya Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa leo kwenye Dimba la CCM Mkwakwani, Jijini Tanga. Bao pekee la Coastal Union kwenye mchezo huo limefungwa na Haji Ugando dakika ya 20 ya mchezo. Katika mchezo huo, Coastal walianza kwa kasi na kufanikiwa kutikisa nyavu dakika ya 4 lakini ilikuwa ni off side, na kisha kupata penati dakika ya 13 lakini Mkwaju wa Mtenje Juma ukapanguliwa na kipa wa Biashara United Balora Nasridine. Biashara United walionekana kumlalamikia mwamuzi wa pembani baada ya kukataa bao lao la dakika ya 45 kwa madai kuwa mfungaji alikuwa ameotea. Mara baada ya mchezo, manahodha wa pande zote mbili wamezungumza. Tazama highlights.