Content removal request!


HIGHLIGHTS & INTERVIEWS: LIPULI FC 1-0 ALLIANCE FC; (TPL - 19/09/2018)

Lipuli FC ya Iringa wameichapa Alliance kutoka Jijini Mwanza bao 1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa leo kwenye dimba la Samora mjini Iringa. Bao pekee la Lipuli limepatikana dakika ya 6 ya mchezo kupitia kwa Miraji Athuman kwa kichwa akiitumia vizuri kros kutoka upande wa kulia. Katika mchezo huo Lipuli walitawala zaidi kipindi cha kwanza kwa mashambulizi mfululizo, lakini Kipindi cha pili alliance waliamka na kuonesha dalili za kusawazisha, lakini haikuwa hivyo. Hata hivyo dakika ya 50, Alliance walifanikiwa kutikisa nyavu za Lipuli lakini mwamuzi akaamua kuwa mfungaji alikuwa off-side na hadi mwisho wa mchezo, Alliance wakaondoka na kipigo hicho cha bao 1-0, kikiwa ni kipigo cha tatu mfululizo. Tazama highlights za mchezo.