Timu ya Mtibwa Sugar ya mkoani Morogoro imeendeleza ushindi katika dimba lake la nyumbani la Manungu baada ya leo kuifunga Mbeya City mabao 2-1 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL). Mara baada ya mchezo huo, Azam TV imezungumza na makocha wa timu zote mbili Ramadhan Swanzurimo wa Mbeya City na Zuberi Katwila wa Mtibwa Sugar, wote wameeleza sababu za kitaalamu za matokeo hayo. Pia Azam TV imezungumza na baadhi ya wachezaji waliong’ara kwenye mchezo huo, Stamili Mbonde ambaye ni mfungaji wa bao la kwanza la Mtibwa, Ismail Aidan Mhesa ambaye ni mfungaji wa bao la pili la Mtibwa na Eric Kyaruzi ambaye ni mfungaji wa bao pekee la Mbeya City.