Subscribes:https://www.youtube.com/c/KidaniStars KIKOSI cha Yanga, leo kimepoteza mchezo wake wa kombe la SportPesa ikiwa ni hatua ya robo fainali kwa kukubali kufungwa mabao 3-2 dhidi ya KK Sharks ya Kenya mchezo uliochezwa Uwanja wa Taifa. Michuano ya SportPesa Cup ambayo kwa sasa ni msimu wake wa tatu imeshirikisha timu nane ikiwa ni nne kutoka Tanzania ambazo ni Singida United, Simba, Mbao na Yanga na zile za kutoka Kenya ni pamoja na KK Sharks, Bandari, AFC Leopards na Gor Mahia ambao ni mabingwa watetezi. Kipindi cha kwanza Yanga walikubali kupoteza kutokana na uzembe wa mabeki ambapo dakika ya 9 KK Sharks waliandika bao la kwanza kupitia kwa Abuye Duke na baada ya kuzidisha mashambulizi wakaandika bao la pili dakika ya 37 kupitia kwa Abege George. Mpaka kipindi cha kwanza kinakamilika Yanga walikuwa nyuma kwa mabao mawili, kipindi cha pili baada ya kufanya mabadiliko kwa kumtoa Haruna Moshi na kuingia Amiss Tambwe pamoja na Abdallah Shaibu na kuingia Thaban Kamusoko, Mrisho Ngassa nafasi yake kuchukuliwa na Deus Kaseke pamoja na Paul Godfery nafasi yake kuchukuliwa na Juma Abdul kasi ya Yanga ilianza kuonekana. Subscribes:https://www.youtube.com/c/KidaniStars Instagram: https://www.instagram.com/kidanistars/ Facebook: https://www.instagram.com/kidanistars/ Twitter: https://twitter.com/kidanistars
Subscribes:https://www.youtube.com/c/KidaniStars MKURUGENZI wa utawala na udhibiti wa SportPesa, Tarimba Abbasi, amezitaka klabu za Simba na Yanga kuacha masihara na badala yake kuhakikisha wanachukua ubingwa wa #SportPesa Super Cup. Kauli hiyo ameitoa leo katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Michuano hiyo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi kesho jijini Dar inahusisha jumla ya timu nane nne za nchini Tanzania ambazo ni Simba, Yanga,Mbao na Singida United na za kutoka Kenya ni Gor Mahia ambaye ni bingwa mtetezi, AFC Leopard, Bandari na KK Sharks. "Haiwezekani tena safari hii ubingwa wa michuano hii uende Kenya kama ilivyofanyika miaka miwili iliyopita, hivyo ni lazima timu za nchini kupambana kuhakikisha wanaubakisha ubingwa hapa nchini. " Tayari nimekutana na viongozi wa Simba, Yanga, Mbao FC na Singida Utd nikiwasisitizia ubingwa ubaki nyumbani. "Nimewaambia waache mzaha kabisa kwa kutumia wachezaji wa vikosi vya pili na badala yake kuwatumia wale wa kikosi cha kwanza. "Mara kadhaa tumeziona Simba na Yanga wakitumia wachezaji wa kikosi cha pili, hivyo mwaka huu hatutaki kitu hicho kitokee kikubwa tunataka ubingwa," alisema Tarimba. Bingwa wa michuano hii anatarajiwa kujichotea dola elfu 30 (Shilingi milioni 70). Subscribes:https://www.youtube.com/c/KidaniStars Instagram: https://www.instagram.com/kidanistars/ Facebook: https://www.instagram.com/kidanistars/ Twitter: https://twitter.com/kidanistars
Mbao FC ya Mwanza leo imepata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mwadui FC kutoka Shinyanga katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. Wenyeji Mbao walitangulia kupata bao dakika ya 7 kupitia kwa Said Khamis Jr, kabla ya Mwadui kusawazisha dakika ya 15 kupitia kwa Salim Aiyee, lakini Pastory Athanas akaihakikishia Mbao pointi tatu baada ya kuifungia bao la pili dakika ya 63 ya mchezo. Baada ya ushindi huo Mbao FC imepanda kutoka nafasi ya 11 hadi nafasi ya 4 ikifikisha pointi 24 huku Mwadui FC ikisalia katika nafasi ileile ya 15 ikiwa na pointi 17.
Mbao FC ya Mwanza leo imepata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mwadui FC kutoka Shinyanga katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. Wenyeji Mbao walitangulia kupata bao dakika ya 7 kupitia kwa Said Khamis Jr, kabla ya Mwadui kusawazisha dakika ya 15 kupitia kwa Salim Aiyee, lakini Pastory Athanas akaihakikishia Mbao pointi tatu baada ya kuifungia bao la pili dakika ya 63 ya mchezo. Baada ya ushindi huo Mbao FC imepanda kutoka nafasi ya 11 hadi nafasi ya 4 ikifikisha pointi 24 huku Mwadui FC ikisalia katika nafasi ileile ya 15 ikiwa na pointi 17.
Vijana wa Azam FC yenye maskani yake Chamazi Jijini Dar es Salaam, wamefanikiwa kuitafuna Mbao FC kwa kuipa kipigo kizito cha mabao 4-0 katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa leo usiku kwenye Dimba la Azam Complex, Chamazi. Mabao ya Azam FC yamefungwa na nahodha wake Agrey Moris dakika ya 37, aliyefunga kwa ‘free-kick’, Joseph Mahindi aliyefunga mabao mawili dakika ya 54 na 58 huku Salum Abubakar ‘sure boy’ akifunga bao la nne dakika ya 63.
Timu ya Mbao FC imelazimika kutoka nyuma na kusawazisha mabao mawili iliyokuwa imefungwa na Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliomalizika kwa sare ya mabao 2-2. Katika mchezo mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza, Mbao ikiwa mwenyeji, Mbeya City imetangulia kupata bao dakika ya 12 kupitia kwa Iddy Selemani Nado, kabla ya Eliud Ambokile kuifungia bao la pili dakika ya 48. Akitokea benchi, Evarigistus Mujwahuki ndiye aliyeifungia Mbao FC mabao yote mawili dakika ya 83 na dakika ya 90+4.
Timu ya Mbao FC imelazimika kutoka nyuma na kusawazisha mabao mawili iliyokuwa imefungwa na Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliomalizika kwa sare ya mabao 2-2. Katika mchezo mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza, Mbao ikiwa mwenyeji, Mbeya City imetangulia kupata bao dakika ya 12 kupitia kwa Iddy Selemani Nado, kabla ya Eliud Ambokile kuifungia bao la pili dakika ya 48. Akitokea benchi, Evarigistus Mujwahuki ndiye aliyeifungia Mbao FC mabao yote mawili dakika ya 83 na dakika ya 90+4. Haya hapa mabao yote.
Mbao FC leo imepata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza. Bao pekee la Mbao limefungwa na Said Khamis Jr dakika ya 48 kwa mtindo wa tikitaka. Litazame.