Vijana wa Azam FC yenye maskani yake Chamazi Jijini Dar es Salaam, wamefanikiwa kuitafuna Mbao FC kwa kuipa kipigo kizito cha mabao 4-0 katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa leo usiku kwenye Dimba la Azam Complex, Chamazi. Mabao ya Azam FC yamefungwa na nahodha wake Agrey Moris dakika ya 37, aliyefunga kwa ‘free-kick’, Joseph Mahindi aliyefunga mabao mawili dakika ya 54 na 58 huku Salum Abubakar ‘sure boy’ akifunga bao la nne dakika ya 63.