Timu ya Mbao FC imelazimika kutoka nyuma na kusawazisha mabao mawili iliyokuwa imefungwa na Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliomalizika kwa sare ya mabao 2-2. Katika mchezo mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza, Mbao ikiwa mwenyeji, Mbeya City imetangulia kupata bao dakika ya 12 kupitia kwa Iddy Selemani Nado, kabla ya Eliud Ambokile kuifungia bao la pili dakika ya 48. Akitokea benchi, Evarigistus Mujwahuki ndiye aliyeifungia Mbao FC mabao yote mawili dakika ya 83 na dakika ya 90+4. Haya hapa mabao yote.