#YANGAvsMBAO MAGOLI YANGA VS MBAO FC 2-0 Yanga imefanikiwa kuapata ushindi wa 2-0 dhidi ya Mbao FC katika uwanja wa Taifa Dar es salaam. Bao la kwanza limepachikwa kimiani na Rafel Daud mnamo dakika ya 16 ya kipindi cha kwanza kwa njia ya kichwa kutokana na mpira wa adhabu uliopigwa na Ibrahim Ajibu. Baada ya kipindi cha kwanza kumalizika, kipindi cha pili Mbao walijitahada kuja kwa kasi kushambulia lango la Yanga lakini haikuweza kusaidia kitu. Licha ya mashambulizi hayo, Mbao FC walipata nafasi zingine kama nne kipindi cha kwanza lakini walishindwa kuzitumia vema. Zikiwa zimeongezwa dakika tano, Ibrahim Ajibu alifanikiwa kuingia kambani kwa kufunga bonge la bao kwa tikitaka ya aina yake na kuifanya Yanga iwe mbele kwa mabao 2-0. Mpaka dakika 90 zinamalizika, Yanga 2 na Mbao FC 0. Matokeo hayo yanaifanya Yanga kufikisha alama 16 katika msimamo wa ligi huku Mbao ikisalia na alama zake 14 kwenye nafasi ya 5. GlobalPublishersApp Android: http://bit.ly/2AAQe1d iOS: http://apple.co/2Assf4M Subscribe http://www.youtube.com/c/uwazi FACEBOOK: https://www.facebook.com/Globalpublis... TWITTER: https://twitter.com/GlobalHabari Visit https://globalpublishers.co.tz/, Subscribe http://www.youtube.com/c/uwazi1 Kupata video nyingine za aina hii, subscribe kwenye chanell yetu kwa kubofya… http://www.youtube.com/c/uwazi1 http://www.youtube.com/c/uwazi1 http://www.youtube.com/c/uwazi1 WEBSITE: https://globalpublishers.co.tz/ FACEBOOKInstall
Simba na Yanga zinakutana kwa mara ya kwanza msimu huu, mchezo ambao endapo Simba ikishinda itafikisha alama 13 na kukwea hadi nafasi ya pili ya msimamo nyuma ya kinara Mbao Fc kwa alama moja. Yanga ikifanikiwa kushinda itafikisha alama 15 na kuongoza ligi mbele ya alama moja dhidi ya Mbao Fc yenye alama 14 mpaka sasa.
Azam FC yavutwa shati nyumbani, Mbao yazidi kutamba kileleni; na kuelekea #SuperSunday ya #KariakooDerby Simba SC na Yanga SC zakaa 'mguu sawa'. TFF yatoa tahadhari kwa mashabiki....ni tahadhari gani? Ungana na Ahmed Abdallah ndani ya MSHIKEMSHIKE VIWANJANI.
Coastal Union ya Jijini Tanga imepata sare ya bao 1-1 na Mbao FC katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa leo kwenye Uwanja wa Mkwakwani Jijini humo. Katika mchezo huo uliokuwa mkali na wa kusisimua, Coastal ndiyo waliotangulia kupata bao kupitia kwa Ayoub Lyanga dakika ya 31 kabla ya Mbao kureje kwa nguvu zaidi kipindi cha pili na kusawazisha kupitia kwa said Hamis Said Jr dakika ya 50. Baada ya mchezo huo makocha wa timu zote mbili Amri Said wa Mbao na Juma Mgunda wa Coastal Union wameuzungumzia mchezo huo
Mchezaji wa Coastal Union ambaye pia ni msanii wa bongo fleva, Alikiba ametegua kitendawili kuhusu siku ambayo ataanza rasmi kucheza kwenye mfululizo wa michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara. Kiba amezungumza na Azam TV mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mbao FC uliopigwa kwenye dimba la Mkwakwani Jijini Tanga na kumalizika kwa sare ya bao 1-1. Katika mahijiano haya pia Alikiba ameichambua timu yake kwa jinsi alivyoutazama mchezo. Mchezaji huyo aliyesajiliwa Coastal Union msimu huu, hajacheza mchezo wowote tangu kuanza kwa ligi hiyo mwishoni mwa mwezi Agosti.
Coastal Union ya Jijini Tanga imepata sare ya bao 1-1 na Mbao FC katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa leo kwenye Uwanja wa Mkwakwani Jijini humo. Katika mchezo huo uliokuwa mkali na wa kusisimua, Coastal ndiyo waliotangulia kupata bao kupitia kwa Ayoub Lyanga dakika ya 31 kabla ya Mbao kureje kwa nguvu zaidi kipindi cha pili na kusawazisha kupitia kwa said Hamis Said Jr dakika ya 50. Haya ndiyo magoli yenyewe
Mbao FC imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons, katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. Bao hilo pekee limepatikana katika dakika ya nne kati ya dakika tano za nyongeza kupitia kwa mshambuliaji wake Ndaki Robert.
Mbao FC imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons, katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. Bao hilo pekee limepatikana katika dakika ya nne kati ya dakika tano za nyongeza kupitia kwa mshambuliaji wake Ndaki Robert. Hili hapa bao lenyewe.