Content removal request!


MBAO FC 2-1 MWADUI FC: HIGHLIGHTS & INTERVIEWS (TPL - 17/12/2018)

Mbao FC ya Mwanza leo imepata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mwadui FC kutoka Shinyanga katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. Wenyeji Mbao walitangulia kupata bao dakika ya 7 kupitia kwa Said Khamis Jr, kabla ya Mwadui kusawazisha dakika ya 15 kupitia kwa Salim Aiyee, lakini Pastory Athanas akaihakikishia Mbao pointi tatu baada ya kuifungia bao la pili dakika ya 63 ya mchezo. Baada ya ushindi huo Mbao FC imepanda kutoka nafasi ya 11 hadi nafasi ya 4 ikifikisha pointi 24 huku Mwadui FC ikisalia katika nafasi ileile ya 15 ikiwa na pointi 17.