Azam FC, imelazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Alliance katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) uliofanyika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam. Ilibidi Azam FC iweze kusubiri hadi dakika ya 79 kuweza kupata bao la uongozi, lililofungwa na Joseph Mahundi, aliyeingia dakika ya 76, kuchukua nafasi ya Ramadhan Singano, na alifunga bao hilo kiustadi akiunganisha krosi ya Chirwa. Dakika ya 90 Alliance ilisawazisha kupitia kwa Dickson Ambundo, akimalizia mpira uliogonga mwamba kufuatia mpira wa adhabu ndogo uliopigwa na Israel Patrick. Azam walionekana kulalamikia bao hilo wakidai kuwa beki wao Agrey Moris alisukumwa kabla ya kufungwa lakini, mwamuzi Abubakar Mturo (Mtwara) na Msaidizi namba moja, Mohamed Mkono (Tanga), waliamuru kuwa bao halali. Mchezo huo ulikuwa na kasi sana, Azam FC ikianza kwa mashambulizi makali langoni mwa Alliance, ambapo dakika ya kwanza Obrey Chirwa, alikosa bao la wazi baada ya kuupiga vibaya mpira akiwa anatazamana na lango ndani ya eneo la hatari, akipokea pasi ya Donald Ngoma. Mabingwa hao waliweza kupata ugumu kuipenya safu ya ulinzi ya Alliance, kutokana na timu hiyo kusimama wengi kujilinda nyuma ya mpira wakati Azam FC ikishambulia. Mara baada ya mchezo huo kumalizika, kipa wa Azam FC, Razak Abalora, alioneshwa kadi nyekundu kufuatia kadi ya pili ya njano iliyosababishwa na lugha ya kutoridhishwa na maamuzi aliyoitoa kwa mwamuzi huyo. Sare hiyo inaifanya Azam FC kufikisha jumla ya pointi 48 katika nafasi ya pili kwenye msimamo ikiwa na mchezo mmoja mkononi, ikizidiwa pointi saba na kinara Yanga aliyefikisha 55 kufuatia suluhu yake ya jana dhidi ya Singida United.
Mabingwa wa Tanzania Bara Simba SC wamepoteza mchezo wao wa kwanza wa raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika (CAF CL) kwa kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Mashetani Wekundu wa Nkana FC katika mchezo uliopigwa mjini Kitwe nchini Zambia. Simba ilionekana kuelemewa zaidi kipindi cha kwanza cha mchezo na kuruhusu bao la kwanza lilifungwa na Ronald Kampamba dakika ya 27 baada ya kazi nzuri iliyofanywa na Hassan Kessy. Kipindi cha pili Simba walionekana kuimarika na kukianza kwa kusukuma mashambulizi langoni kwa Nkana lakini walijikuta wakifanya makosa katika safu yao ya ulinzi na kuruhusu bao la pili, lililotiwa kimiani na Kelvin Kampamba dakika ya 56. Simba walipata bao lao pekee dakika ya 73 kwa mkwaju wa penati uliofungwa na Nahodha wao John Bocco baada ya Meddie Kegere kuangushwa ndani ya eneo la hatari. Kwa matokeo hayo sasa Simba itahitaji ushindi wa kuanzia bao 1-0 katika mchezo wa marudiano utakaopigwa Jijini Dar es Salaam, wiki moja ijayo.
Bao la pili la Singida United likiwekwa kimiani na Tibar George baada ya walinzi wa Mbeya City kufanya uzembe wa kutoondoa hatari langoni mwao. Tazama bao hilo
UGANDA VS TANZANIA 0 -0 Kikosi cha Taifa Stars, kimelazimishwa sare ya bila kufungana kikiwa ugenini dhidi ya wenyeji wake Uganda. Mechi hiyo ya kuwania kufuzu Afcon imepigwa kwenye Uwanja wa Namboole jijini Kampala na Stars iliyokuwa ikiongozwa na nahodha Mbwana Samatta imeonyesha soka safi na kuwapa wakati mgumu Uganda. Stars ilifanya mashambulizi mengi zaidi langoni mwa Uganda, hasa katika kipindi cha pili, hali iliyowalazimisha walinzi wa Uganda kufanya faulo nyingi zaidi. Kipindi cha kwanza ilionekana Uganda wakiwa na nafasi nyingi ambazo hawakuzitumia huku mvua kubwa iliyonyesha dakika chache kabla ya mechi ikiwa imechangia kuvurugika kwa uwanja huo. Install GlobalPublishersApp Android: http://bit.ly/2AAQe1d iOS: http://apple.co/2Assf4M Subscribe http://ww.youtube.com/c/uwazi FACEBOOK: https://www.facebook.com/Globalpublis... TWITTER: https://twitter.com/GlobalHabari Visit https://globalpublishers.co.tz/, Suazi1 http://www.youtube.com/c/uwazi1 WEBSITE: https://globalpublishers.co.tz/ FACEBOOK: https://www.facebook.com/Globalpublis... TWITTER: https://twitter.com/GlobalHabari INSTAGRAM: https://www.instagram.com/globalpubli..SSI
Timu ya Mbao FC ya jijini Mwanza imepanda hadi nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa ligi kuu soka Tanzania bara baada ya kufanikiwa kutoa suluhu na Singida United katika mchezo uliopigwa jioni ya leo kwenye dimba la Namfua mkoani Singida. Singida United ambao walikuwa nyumbani wakisaka ushindi ambao utawasaidia kuweka katika nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi walijikuta katika wakati mgumu dhidi ya walinzi wa timu ya Mbao FC waliokuwa wakiondosha hatari zilizokuwa zikielekezwa langoni mwao. Matokeo hayo yamekuwa mazuri kwa upande wa Mbao FC waliokuwa ugenini kwa kuwa wamefikisha alama 7 na kuwa nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa ligi kuu baada ya kushinda michezo miwili na kutoa suluhu mchezo mmoja. Wakati Singida United katika michezo mitatu ya ligi waliocheza Namfua msimu huu wamefanikiwa kushinda mchezo mmoja, kupoteza mchezo mmoja na suluhu mchezo mmoja.
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara Simba SC wameanza kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons, katika mchezo uliopigwa kwenye Dimba la Taifa Dar es Salaam. Bao pekee la Simba kwenye mchezo huo limefungwa na mshambuliaji wake mpya Meddie Kagere dakika ya 2 ya mchezo akitumia vyema pasi ya kisigino kutoka kwa nahodha wake, John Bocco. Licha ya Simba kutawala zaidi mchezo, kipindi cha kwanza, Wajelajela Tanzania Prisons walionekana kuwa na ukuta imara zaidi kudhidibiti mashambulizi ya mara kwa mara kutoka kwa Simba, hali iliyowafanya wasiruhusu bao lingine. Kipindi cha pili Tanzania Prisons walionekana kuimarika zaidi na kusukuma mashambulizi langoni kwa Simba huku wakitawala zaidi katikati, lakini umiliki wao haukuwa na madhara yoyote kwa Simba, na hadi dakika 90 zinakamilika, Simba wakafanikiwa kuondoka na alama tatu muhimu kutoka dimba la nyumbani.
Timu ya Ruvu Shooting leo ikiwa kwenye uwanja wake wa nyumbani wa Mabatini mkoani Pwani, imeambulia sare ya kufungana goli 1-1 na Mwadui FC katika mchezo pekee wa raundi ya 27 ya Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL) ambayo imeanza hii leo. Katika mchezo huo mchezaji Abdallah Seseme wa Mwadui FC ameweka rekodi ya kufunga bao la mapema zaidi kwenye ligi hiyo msimu huu alipoitanguliza timu yake kwa bao la sekunde ya 12 ya mchezo. Baada ya kufungwa bao hilo, Ruvu waliongeza kasi ya mashambulizi lakini hadi kipindi cha kwanza kinamalizika walikuwa nyuma kwa bao hilo moja. Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kwa Ruvu kushambulia mfululizo na hatimaye kupata bao la kusawazisha dakika ya 69 kupitia kwa Fully Maganga baada ya kutokea piga nikupige langoni kwa Mwadui FC. Matokeo hayo yanaifanya Ruvu Shooting kusogea hadi nafasi ya saba ikifikisha pointi 33 huku Mwadui ikibaki nafasi yake ya tisa ikiwa na pointi 30.
Katika mchezo huo uliokuwa mbashara Azam Sports 2, Mtibwa Sugar ikiwa katika ubora wake, imeitandika Singida United magoli 3-0. Magoli ya Mtibwa yamefungwa na Kelvin Sabato ‘Kiduku’ aliyefunga goli la kwanza kwa mpira wa adhabu ndogo (free kick) dakika ya 22 ya mchezo na hadi kipindi cha kwanza kinamalizika, Mtibwa walikuwa mbele kwa bao hilo. Kipindi cha pili kilianza kwa Mtibwa kuzidisha moto langoni kwa Singida na hatimaye kupata bao la pili dakika ya 53 kupitia kwa Salum Kihimbwa akimlizia pasi ya Hassan Dilunga, huku Dilunga mwenyewe akiweka wavuni bao la tatu kwa mkwaju wa penati dakika ya 71.