Katika mchezo huo uliokuwa mbashara Azam Sports 2, Mtibwa Sugar ikiwa katika ubora wake, imeitandika Singida United magoli 3-0. Magoli ya Mtibwa yamefungwa na Kelvin Sabato ‘Kiduku’ aliyefunga goli la kwanza kwa mpira wa adhabu ndogo (free kick) dakika ya 22 ya mchezo na hadi kipindi cha kwanza kinamalizika, Mtibwa walikuwa mbele kwa bao hilo. Kipindi cha pili kilianza kwa Mtibwa kuzidisha moto langoni kwa Singida na hatimaye kupata bao la pili dakika ya 53 kupitia kwa Salum Kihimbwa akimlizia pasi ya Hassan Dilunga, huku Dilunga mwenyewe akiweka wavuni bao la tatu kwa mkwaju wa penati dakika ya 71.