Content removal request!


HIGHLIGHTS: RUVU SHOOTING 1-1 MWADUI FC (VPL - 04/05/2018

Timu ya Ruvu Shooting leo ikiwa kwenye uwanja wake wa nyumbani wa Mabatini mkoani Pwani, imeambulia sare ya kufungana goli 1-1 na Mwadui FC katika mchezo pekee wa raundi ya 27 ya Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL) ambayo imeanza hii leo. Katika mchezo huo mchezaji Abdallah Seseme wa Mwadui FC ameweka rekodi ya kufunga bao la mapema zaidi kwenye ligi hiyo msimu huu alipoitanguliza timu yake kwa bao la sekunde ya 12 ya mchezo. Baada ya kufungwa bao hilo, Ruvu waliongeza kasi ya mashambulizi lakini hadi kipindi cha kwanza kinamalizika walikuwa nyuma kwa bao hilo moja. Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kwa Ruvu kushambulia mfululizo na hatimaye kupata bao la kusawazisha dakika ya 69 kupitia kwa Fully Maganga baada ya kutokea piga nikupige langoni kwa Mwadui FC. Matokeo hayo yanaifanya Ruvu Shooting kusogea hadi nafasi ya saba ikifikisha pointi 33 huku Mwadui ikibaki nafasi yake ya tisa ikiwa na pointi 30.