Content removal request!


HIGHLIGHTS & INTERVIEWS: SINGIDA UNITED 0-0 MBAO FC (TPL 31/08/2018)

Timu ya Mbao FC ya jijini Mwanza imepanda hadi nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa ligi kuu soka Tanzania bara baada ya kufanikiwa kutoa suluhu na Singida United katika mchezo uliopigwa jioni ya leo kwenye dimba la Namfua mkoani Singida. Singida United ambao walikuwa nyumbani wakisaka ushindi ambao utawasaidia kuweka katika nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi walijikuta katika wakati mgumu dhidi ya walinzi wa timu ya Mbao FC waliokuwa wakiondosha hatari zilizokuwa zikielekezwa langoni mwao. Matokeo hayo yamekuwa mazuri kwa upande wa Mbao FC waliokuwa ugenini kwa kuwa wamefikisha alama 7 na kuwa nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa ligi kuu baada ya kushinda michezo miwili na kutoa suluhu mchezo mmoja. Wakati Singida United katika michezo mitatu ya ligi waliocheza Namfua msimu huu wamefanikiwa kushinda mchezo mmoja, kupoteza mchezo mmoja na suluhu mchezo mmoja.