Hatimaye Yanga imefanikiwa kuwashika mahasimu wake Simba SC kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL) kwa kufikisha pointi 46, huku ikiendelea kubaki nafasi ya pili kwa tofauti ya mabao, licha ya Simba kuwa na kiporo cha mchezo mmoja mkononi. Yanga imefanikiwa kufikia hatua hiyo baada ya kuichapa Stand United kutoka Shinyanga jumla ya mabao 3-1 katika mchezo wa raundi ya 22 wa ligi hiyo uliopigwa leo kwenye dimba la Taifa jijini Dar es Salaam. Magoli ya Yanga yamefungwa na Ally Ally likiwa ni la kujifunga dakika ya 7, Ibrahim Ajib dakika ya 12 na Obrey Chirwa dakika ya 85 wakati bao pekee la Stand likifungwa na Vitalis Mayanga dakika ya 82. Hata hivyo Stand United watajilaumu wenyewe kwa kupoteza nafasi za wazi zaidi ya tano kwa washambuliaji wake kutokuwa makini kila wanapofika langoni kwa Yanga. Tazama kwa ufupi jinsi mambo yalivyokuwa.
Akiwa ametokea benchi, mshambuliaji raia wa Ghana, Bernard Arthur ameifungia Azam bao la pili akitumia makosa ya kipa wa Mbao ambaye alitoka langoni mapema. FT: Azam FC 2-1 Mbao FC
Azam FC imeendelea kuutumia vyema uwanja wake wa nyumbani wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar es Salaam, baada ya leo kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mwadui FC kutoka mjini Shinyanga, katika mchezo wa raundi ya 21 ya Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL) uliopigwa leo Machi 8, 2018. Ushindi huu ni wa pili mfululizo katika dimba la hilo baada ya kuichapa Singida United bao 1-0 mchezo uliopigwa wiki iliyopita. Bao pekee la Azam katika mchezo huo limepachikwa na Yahya Zayd dakika ya tano ya mchezo akitumia makosa ya golikipa wa Mwadui FC, Anold Massawe alishindwa kutuliza mpira aliorejeshewa na beki wake Iddy Mfaume. Katika mchezo huo Mwadui FC imeonesha kiwango kizuri kwa kufanya mashambulizi mashambulizi ya nguvu langoni mwa Azam, lakini haikuwa na bahati na hatimaye kukubali kupoteza mchezo huo.
Please watch: "MAGOLI YOTE YA SIMBA 5 - 0 MBAO" https://www.youtube.com/watch?v=lU7L3hP4BP0 --~-- SIMBA SC imezidi kuwaacha mbali wapinzani katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Azam FC jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Hongera kwake mfungaji wa bao pekee la leo, mshambuliaji Mganda Emmanuel Arnold Okwi aliyefunga dakika ya 36 baada ya kutokea patashika kwenye lango la Azam FC kufuatia krosi ya beki Mghana, Asante Kwasi. Simba SC sasa inafikisha pointi 41 baada ya kucheza mechi 17, wakiwazidi kwa pointi saba, mabingwa watetezi, Yanga SC wenye pointi 34 katika nafasi ya pili na Azam FC wanabaki nafasi ya tatu kwa pointi zao 33. Dalili za Simba inayofundishwa na kocha Mfaransa, Pierre Lechantre anayesaidiwa na Mrundi, Masoud Juma kupata bao zilionekana mapema tu mchezo huo ulipoanza kutokana na mashambulizi yake mfululizo langoni mwa wapinzani. Azam FC walizidiwa katika safu ya kiungo na kujikuta wanawapa fursa Simba kutawala mchezo sehemu kubwa ya kipindi cha kwanza. Benchi la Ufundi la Azam chini ya Mromania, Aristica Cioaba ba mzalendo, Iddi Cheche liliona hilo na mapema kipindi cha pili wakamuingiza kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’ kwenda kuchukua nafasi ya mshambuliaji Iddi Kipagwile. Mabadiliko hayo yaliipa uhai Azam FC na kuanza kupeleka mashambulizi makali langoni mwa Simba, lakini kipa namba moja nchini, Aishi Manula alisimama imara kuokoa akisaidiwa na mabeki, Yussuph Mlipili na Erasto Nyoni. Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Aishi Manula, Shomary Kapombe, Erasto Nyoni, Yussuph Mlipili, Asante Kwasi, Jonas Mkude, Shiza Kichuya, Said Ndemla/Muzamil Yassin dk59, John Bocco, Emmanuel Okwi/Nicholaus Gyan dk84 na James Kotei. Azam FC; Razak Abalora, Daniel Amoah, Bruce Kangwa, Yakubu Mohammed, Aggrey Morris, Stephan Kingue, Iddi Kipagwile/Salum Abubakar ‘Sure Boy’ dk55, Frank Domayo, Mbaraka Yussuph, Yahya Zayed/Bernard Arthur dk71 na Enock Atta-Agyei.
Please watch: "MAGOLI YOTE YA SIMBA 5 - 0 MBAO" https://www.youtube.com/watch?v=lU7L3hP4BP0 --~-- MSHAMBULIAJI Mganda Emmanuel Arnord Okwi ametokea benchi na kufunga mabao mawili Simba SC ikishinda 4-0 dhidi ya Singida United katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Matokeo hayo yanaifanya Simba SC ifikishe pointi 29, baada ya kucheza mechi 13, ikiwazidi pointi saba mabingwa watetezi, Yanga SC na pointi mbili Azam FC wenye 27 katika nafasi ya pili, wakati Mtibwa Sugar sasa ni ya tatu kwa pointi zae 24 baada ya timu zote kucheza mechi 13. Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Jacob Adongo wa Mara, aliyesaidiwa na Mohammed Mkono wa Tanga na Gasper Ketto wa Arusha hadi mapumziko Simba SC walikuwa wanaongoza kwa mabao 2-0. Kiungo Shiza Ramadhani Kichuya alianza kuifungia Simba SC dakika ya tatu akimalizia mpira wa adhabu uliopigwa na kiungo mkongwe Mwinyi Kazimoto, kufuatia John Raphael Bocco kuangushwa nje kidogo ya boksi. Singida wakacharuka na kuanza kupeleka mashambulizi mfululizo langoni mwa Simba kusaka bao la kusawazisha, lakini ngome ya Wekundu wa Msimbazi ikiongozwa na Erasto Edward Nyoni ilikuwa imara kuondosha hatari zote. Beki Mghana, Asante Kwasi akaifungia Simba SC bao la pili dakika ya 25 akimvisha kanzu kipa Peter Manyika aliyetoka langoni bila hesabu nzuri baada ya pasi ndefu ya kiungo Said Ndemla aliyetokea benchi kuchukua nafasi ya Kazimoto. Bao hilo lilionekana kuwachanganya Singida United wanaofundishwa na kocha Mholanzi, Hans van der Pluijm na kuwaruhusu Simba kutawala zaidi mchezo huo. Kipindi cha pili, mashabiki wa Simba SC wakaripuka kwa shangwe baada ya kumuona kocha wao mpya, Mfaransa Pierre Lechantre aliyeongozana na msaidizi wakea, kocha wa viungo, Mmorocco Mohammed Aymen Hbibi jukwaa kuu. Kocha huyo amekuja kusaini mkataba wa kuifundisha Simba kuchukua nafasi ya Mcameroon, Joseph Marius Omog aliyeondolewa Desemba na atafanya kazi na Mrundi, Masudi Juma ambaye amekuwa akiiongoza tangu kipindi chote hiki. Okwi akatokea benchi dakika ya 65 kuchukua nafasi ya kiungo Muzamil Yassin na akafunga mabao mawili ndani ya dakika saba. Alifunga bao la tatu dakika ya 75 akimalizia pasi ya Shiza Kichuya na la nne dakika ya 82 akimalizia pasi ya Ndemla. Alifunga mabao hayo, baada ya kumsetia pasi nzuri Kichuya, akapiga nje akiwa ndani ya sita. Kikosi cha Simba SC leo kilikuwa; Aishi Manula, Nicholas Gyan, Asante Kwasi, Juuko Murshid, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, James Kotei/Mohammed Ibrahim dk88, Mwinyi Kazimoto/Said Ndemla dk22, John Bocco, Shiza Kichuyana Muzamil Yassin/Emmanuel Okwi dk65. Singida United; Peter Manyika, Michael Rusheshangoga, Shafiq Batambuze, Kennedy Wilson, Malik Antiri, Mudathir Yahya, Deus Kaseke, Tafadzwa Kutinyu/Yussuf Kagoma79, Lubinda Mundia/Kenny Ally76, Kambale Salita Gentil na Kiggi Makassy/Salum Chukwu dk62.