Kipindi hiki cha Februari 28, kimechambua matukio kadhaa yenye utata katika mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara, likiwemo lile la Simba kupewa penati katika mchezo wao dhidi ya African Lyon uliopigwa Februari 19 mwaka huu kwenye Dimba la Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha. Tazama ni kwanini kipindi hiki kimesema kuwa penati ile haikuwa halali. Matukio mengine ni ya off-side, ambapo katika wiki hiyo mhanga mkubwa amekuwa ni Stand United aliyenyimwa magoli mawili halali kwenye mchezo wake na Mbeya City uliopigwa kwenye Uwanja wa Sokoine Mbeya kwa kigezo cha off-side. Matukio mengine ni kwenye mchezo kati ya Azam FC dhidi ya Simba, Lipuli FC dhidi ya Azam FC, pamoja na mchzo wa Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC) kati ya KMC na Mtibwa Sugar ambapo kuna penati ilirudiwa. Tupo na waamuzi wastaafu Osman Kazi na Manyama Bwire. #KipyengaChaMwisho ni kila Alhamisi saa 3:30 usiku #AzamSports2
Watani wa Jadi Yanga na Simba walikutana Jumamosi ya tarehe 16, Februari kwenye Uwanja wa Taifa ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ukichezeshwa na mwamuzi Hance Mabena. Kwa mujibu wa waamuzi wastaafu Osman Kazi na Manyama Bwire, mwamuzi huyo alichezesha vizuri kwa sehemu kubwa licha ya mapungufu machache ya kibinadamu ikiwemo kuinyima Simba penati kufuatia tukio lililotokea dakika ya 49 kati ya Abdallah Shaibu na John Bocco. Je, ni maeneo gani alipatia na maeneo gani alikosea? Tazama kipindi hiki kilichoruka Alhamis ya tarehe 21/02/2019 Azam Sports 2.
Katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa Novemba 23, 2018 kuna matukio kadhaa yaliyozua utata, kubwa likiwa ni bao alilofunga Meddie Kagere, lakini ikaamuliwa kuwa alikuwa off-side. Kwa mujibu wa Kipyenga cha Mwisho cha Azam Sports chini ya mwamuzi mstaasu Osman Kazi na Mkufunzi wa waamuzi Hemed Mteza, goli lile lilikuwa halali. Mbali na tukio hilo pia palikuwa na tukio lingine la Simba kunyimwa penati halali pamoja na matukio ya off-side. Yote haya ni kwenye kipindi cha Kipyenga cha Mwisho ambacho hukufikia kila Alhamis, saa 3;30 usiku Azam Sports 2.
Kwa mujibu wa kipindi hiki cha terehe 08/11/2018, bao la pili alilofunga Meddie Kagere kwenye mchezo kati ya JKT Tanzania vs Simba SC uliopigwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga Jumamosi ya Novemba 2, 2018, halikuwa bao halali kwa kuwa mfungaji alikuwa ameotea kabla ya kufunga. Pamoja na matukio mengine yaliyojiri kwenye mchezo huo, pia palikuwa na matukio mawili ya wachezaji wa JKT kudai penati wakidai wachezaji wa Simba Mohamed Hussein na Erasto Nyoni kwa nyakati tofauti, walishika mpira ndani ya eneo la hatari hadi kusababisha mchezaji wa JKT Ahmed Shiboli kutolewa nje kwa kadi nyekundu. Mbali na mchezo huo, kipindi hiki kimechambua mechi kdhaa za raundi ya 13 ya Ligi Kuu Tanzania Bara ukiwemo mchezo wa Yanga vs Ndanda SC na ule wa Kagera Sugar vs Azam FC. Tukio kubwa katika mchezo wa Kagera Sugar na Azam FC ni mchezaji wa Azam FC Donald Ngoma kupewa kadi nyekundu, kadi ambayo wengi hawakuelewa sababu za adhabu hiyo kumkumba. Waamuzi wawili wastaafu ambao ni magwiji, Osman Kazi na Omary Abdulkadir wamechambua matukio yote na kuonesha ni wapi waamuzi walikosea na wapi waamuzi walipatia, na nini walipaswa kufanya. Kipyenga cha Mwisho ni kila Alhamis saa 3:30 usiku Azam Sports 2.
Miongoni mwa taarifa zilizomo ni pamoja na ripoti kamili kuhusu yaliyojiri kwenye mechi tatu za Ligi Kuu tanzania Bara zilizopigwa leo, pamoja na maoni ya mashabiki. Pia Mwanachama wa Simba Chuma Suleiman Mzee maarufu kama Bi Hindu ametoa tambo zake kuelekea mchezo wa Watani wa jadi Septe 30, 2018. Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi ametoa sifa na vigezo kwa waamuzi watakaochezesha mchezo wa Watani wa jadi Simba na Yanga Septemba 30. Pamoja na mengine mengi ungana na Ahmed Abdallah. Kumbuka kipindi hiki ni kila siku saa 3:00 usiku Azam Sports 2.
Msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) 2018/19 umeanza kwa lawama lukuki kwa waamuzi katika baadhi ya michezo wakidaiwa kukataa magoli ya timu mbalimbali kwa madai kuwa wafungaji walikuwa wameotea. Baadhi ya mechi zilizolalamikiwa ni ile ya Yanga vs Mtibwa Sugar, Coastal Union Vs Biashara United, Ruvu Shooting vs KMC na Alliance vs Mbao FC ikiwa ni raundi mbili pekee zimeshachezwa tangu kuanza kwa msimu huo. Suala hilo la kutafsiri sharia ya ‘off-side’ linachambuliwa kwa kina na Osman Kazi kupitia kipindi cha Kipyenga cha Mwisho cha wiki hii, Alhamisi Agosti 30, 2018. Kipyenga cha mwisho ni kila Alhamisi, saa 1:00 usiku LIVE Azam Sports 2.