Msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) 2018/19 umeanza kwa lawama lukuki kwa waamuzi katika baadhi ya michezo wakidaiwa kukataa magoli ya timu mbalimbali kwa madai kuwa wafungaji walikuwa wameotea. Baadhi ya mechi zilizolalamikiwa ni ile ya Yanga vs Mtibwa Sugar, Coastal Union Vs Biashara United, Ruvu Shooting vs KMC na Alliance vs Mbao FC ikiwa ni raundi mbili pekee zimeshachezwa tangu kuanza kwa msimu huo. Suala hilo la kutafsiri sharia ya ‘off-side’ linachambuliwa kwa kina na Osman Kazi kupitia kipindi cha Kipyenga cha Mwisho cha wiki hii, Alhamisi Agosti 30, 2018. Kipyenga cha mwisho ni kila Alhamisi, saa 1:00 usiku LIVE Azam Sports 2.