Azam FC ilivyoiondoa Yanga nafasi ya pili kwa kuichapa Mwadui bao 1-0 - March 8, 2018
Azam FC ilivyoiondoa Yanga nafasi ya pili kwa kuichapa Mwadui bao 1-0 - March 8, 2018

KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, imefanya kweli baada ya kuidungua Mwadui bao 1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) uliomalizika Uwanja wa Azam Complex usiku huu. Ushindi huo unaifanya Azam FC kusogea hadi nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ikifikisha jumla ya pointi 41 na kuishusha Yanga yenye mechi mbili mkononi hadi nafasi ya nne ikibakiwa na pointi zao 40 huku Simba ikiwa kileleni kwa pointi 46. Bao pekee la Azam FC limewekwa kimiani na mshambuliaji Yahya Zayd, dakika ya tano akitumia uzembe wa kipa wa Mwadui, Anold Massawe, aliyepiga mpira vibaya na kumpasia mguuni mfungaji wakati akiwa kwenye harakati za kuupiga mbele mpira aliorudishiwa na beki wake, Idd Mfaume.



Jinsi Ruvu Shooting 'walivyoipapasa' Mtibwa Sugar, dimba la Manungu
Jinsi Ruvu Shooting 'walivyoipapasa' Mtibwa Sugar, dimba la Manungu

Ni katika dimba la Manungu mkoani Morogoro, ambapo Ruvu Shooting imeendeleza wimbi la ushindi baada ya kuwalaza mabao 2-1 wenyeji wao Mtibwa Sugar na kupanda mpaka nafasi ya saba ya msimamo wa VPL ikifikisha alama 23, nyuma ya wapinzani wao Mtibwa wenye alama 27 kwenye nafasi ya sita



SIMBA HII  NI BALAA,YAINYOA AZAMFC 1-0
SIMBA HII NI BALAA,YAINYOA AZAMFC 1-0

Simba imeibuka na ushindi wa goli moja kwa sifuri katika mchezo wa VPL uliofanyika uwanja mkubwa wa Taifa na kuzidi kujichimbia kileleni mwa msimamo wa VPL



Goli la Okwi lililoidhoofisha Azam FC vs Simba katika mbilio za Ubingwa VPL
Goli la Okwi lililoidhoofisha Azam FC vs Simba katika mbilio za Ubingwa VPL

Baada ya headlines na shauku ya mashabiki wengi kutaka kushuhudia game ya Simba na Azam FC nani atakuwa mbabe, hatimae leo Jumatano ya February 7 2018 game hiyo imechezwa na mbabe amejulikana. Game ya Simba dhidi ya Azam FC leo ilikuwa na ushindani mkubwa kutokana na timu hizo zote hizo kufukuzana kwa karibu hivyo matokeo ya mchezo huo yalikuwa yanatarajiwa kuleta taswira mpya katika msimamo wa Ligi, hivyo kupoteza Azam FC kwa goli 1-0 kumeanza kuikatisha tamaa Azam FC katika mbio za Ubingwa kwa kuachwa point nane.



Kocha Wa Ruvu Shooting Ataka Kulia Kufungwa Bao 3-0 dhidi Ya Simba!
Kocha Wa Ruvu Shooting Ataka Kulia Kufungwa Bao 3-0 dhidi Ya Simba!

SUBSCRIBE: https://www.youtube.com/c/KidaniStars Ligi kuu Tanzania bara imeendelea kwa michezo kadhaa iliyochezwa viwanja tofauti lakini jicho lilikuwa uwanja wa Uhuru kushuhudia mchezo kati ya Ruvu Shooting dhidi ya Simba ambao umemalizika na kuishuhudia simba ikiiadhibu Ruvu Shooting kwa magoli 3-0 na kuendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi. SUBSCRIBE: https://www.youtube.com/c/KidaniStars Magoli ya Simba yamefungwa na John Bocco ambaye amefungaagoli mawili dakika ya 22 na 75, Mzamiru Yassin alifunga goli moja dakika ya 66. SUBSCRIBE: https://www.youtube.com/c/KidaniStars SUBSCRIBE: https://www.youtube.com/c/KidaniStars SUBSCRIBE: https://www.youtube.com/c/KidaniStars SUBSCRIBE: https://www.youtube.com/c/KidaniStars



Simba mwendo mdundo VPL,Yaipiga Ruvu Shooting3-0
Simba mwendo mdundo VPL,Yaipiga Ruvu Shooting3-0

Simba imeendelea kujichimbia kileleni mwa msimamo wa vpl baada ya kuchomoza na ushindi wa 3-0 dhidi ya Ruvu Shooting ktk uwanja wa Uhuru



Simba yaichapa Kagera sugar 2-0,Nyoso akamatwa
Simba yaichapa Kagera sugar 2-0,Nyoso akamatwa

Simba imerejea kileleni mwa msimamo wa VPL baada ya kuichapa magoli 2-0 timu ya Kagera sugar katika uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera. Baada ya mchezo huo,Mchezaji wa Kagera sugar Juma Saidi Nyoso alimpiga shabiki wa Simba hadi kuzimia ambapo alikimbizwa hospitali na Nyoso kushikiliwa na polisi.



SIMBA Yainyoa Singida united, Yamtangaza Kocha
SIMBA Yainyoa Singida united, Yamtangaza Kocha

Simba imeichapa timu ngumu ya Singida united magoli manne kwa sifuri katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara maarufu kama VPL na kujichimbia kileleni mwa msimamo wa ligikuu. Wakati huohuo timu hiyo imemtangaza Kocha mpya atakayeinoa timu hiyo.




« Previous Next »


Popular Tags

#Goalkeeper Saves  #Kevin Durant  #Football Defensive Skills  #Football Skills  #Kawhi Leonard  #Paul George  #Russell Westbrook  #Paul Pogba  #Best Goals  #Counter Attack Goals Football  

Popular Users

#rogerfederer  #UKCoachCalipari  #TimTebow  #cnnbrk  #nytimes  #geniebouchard  #serenawilliams  #_BAnderson30_  #SimplyAJ10  #nfl  #sydneyleroux  #hunterpence  #billsimmons