Baada ya headlines na shauku ya mashabiki wengi kutaka kushuhudia game ya Simba na Azam FC nani atakuwa mbabe, hatimae leo Jumatano ya February 7 2018 game hiyo imechezwa na mbabe amejulikana. Game ya Simba dhidi ya Azam FC leo ilikuwa na ushindani mkubwa kutokana na timu hizo zote hizo kufukuzana kwa karibu hivyo matokeo ya mchezo huo yalikuwa yanatarajiwa kuleta taswira mpya katika msimamo wa Ligi, hivyo kupoteza Azam FC kwa goli 1-0 kumeanza kuikatisha tamaa Azam FC katika mbio za Ubingwa kwa kuachwa point nane.