Simba VS Yanga Mashabiki wa Simba na Yanga Wacharuka Taifa
Simba VS Yanga Mashabiki wa Simba na Yanga Wacharuka Taifa

Simba na Yanga zinakutana kwa mara ya kwanza msimu huu, mchezo ambao endapo Simba ikishinda itafikisha alama 13 na kukwea hadi nafasi ya pili ya msimamo nyuma ya kinara Mbao Fc kwa alama moja. Yanga ikifanikiwa kushinda itafikisha alama 15 na kuongoza ligi mbele ya alama moja dhidi ya Mbao Fc yenye alama 14 mpaka sasa.



HIGHLIGHTS & INTERVIEWS: SINGIDA UNITED 0-0 MBAO FC (TPL 31/08/2018)
HIGHLIGHTS & INTERVIEWS: SINGIDA UNITED 0-0 MBAO FC (TPL 31/08/2018)

Timu ya Mbao FC ya jijini Mwanza imepanda hadi nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa ligi kuu soka Tanzania bara baada ya kufanikiwa kutoa suluhu na Singida United katika mchezo uliopigwa jioni ya leo kwenye dimba la Namfua mkoani Singida. Singida United ambao walikuwa nyumbani wakisaka ushindi ambao utawasaidia kuweka katika nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi walijikuta katika wakati mgumu dhidi ya walinzi wa timu ya Mbao FC waliokuwa wakiondosha hatari zilizokuwa zikielekezwa langoni mwao. Matokeo hayo yamekuwa mazuri kwa upande wa Mbao FC waliokuwa ugenini kwa kuwa wamefikisha alama 7 na kuwa nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa ligi kuu baada ya kushinda michezo miwili na kutoa suluhu mchezo mmoja. Wakati Singida United katika michezo mitatu ya ligi waliocheza Namfua msimu huu wamefanikiwa kushinda mchezo mmoja, kupoteza mchezo mmoja na suluhu mchezo mmoja.



Manara Yanga walipatwa na Bumbuwazi mechi yao na Asante Kotoko
Manara Yanga walipatwa na Bumbuwazi mechi yao na Asante Kotoko

Uongozi wa klabu ya Simba umetangaza rasmi kucheza na timu ya Asante Kotoko ya Ghana katika tamasha lake la Simba Day, Agosti 8 mwaka huu. Kupitia kwa Ofisa Habari wa klabu hiyo, Haji Sunday Manara, amesema Simba itachuana na timu hiyo kongwe ambayo inashiriki Ligi Kuu Ghana kwa ajili ya kuitambulisha timu yao. Manara amewatangaza Kotoko kucheza nao baada ya hapo awali kuenea kwa taarifa kuwa Simba imewaalika wapinzani wakubwa wa Gor Mahia FC, AFC Leopards kutoka Kenya lakini amezikanusha akisema hazikuwa na ukweli. Katika msimamo wa Ligi Kuu Ghana, Kotoko wamecheza mechi 15 wakiwa kwenye nafasi ya 4 huku wakijikusanyia alama 24 na Ashanti Gold iliyo nafasi ya kwanza ina alama 27 ikiwa imecheza michezo 15 pia. Zikiwa zimesalia siku 7 pekee kuelekea tamasha hilo, kikosi cha Simba hivi sasa kipo katika kambi maalum ya wiki mbili nchini Uturuki ambapo kimeweka kambi katika jiji la Instanbul. Kikosi hicho baada ya kambi yake kumalizika kitaanza safari ya kurejea nchini kuanzia tarehe 4 mwezi huu tayari kwa tamasha hilo kubwa linalofanyika kila mwaka.



SIMBA VS NDANDA 1-0 ,GOLI la Okwi Lililoipa Simba Points Tatu
SIMBA VS NDANDA 1-0 ,GOLI la Okwi Lililoipa Simba Points Tatu

SIMBA VS NDANDA 1-0 ,GOLI la Okwi Lililoipa Simba Points Tatu Kikosi cha Simba kimeendelea kuunusa ubingwa wa Ligi Kuu kwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ndanda FC. Bao pekee katika mchezo huo limetiwa kimiani na Mshambuliaji wa kimataifa, Mganda, Emmanuel Okwi. Okwi alifunga bao hilo baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa beki wa kulia, Shomari Kapombe. Matokeo hayaifanya Simba ifikishe alama 65 kwenye msimamo wa ligi huku Ndanda FC wakisalia kwenye nafasi 15 wakiwa na alama 23. lnstal GlobalPublishersApp Android: http://bit.ly/2AAQe1d iOS: http://apple.co/2Assf4M Subscribe http://www.youtube.com/c/uwazi FACEBOOK: https://www.facebook.com/Globalpublis... TWITTER: https://twitter.com/GlobalHabari Visit https://globalpublishers.co.tz/, Subscribe http://www.youtube.com/c/uwazi1 kupata video nyingine za aina hii, subscribe kwenye chanell yetu kwa kubofya… http://www.youtube.com/c/uwazi1 http://www.youtube.com/c/uwazi1 http://www.youtube.com/c/uwazi1 WEBSITE: https://globalpublishers.co.tz/ FACEBOOK: https://www.facebook.com/Globalpublis... TWITTER: https://twitter.com/GlobalHabari INSTAGRAM: https://www.instagram.com/globalpubli..



HIGHLIGHTS: MWADUI FC 1-0 MBAO FC (VPL - 30/04/2018)
HIGHLIGHTS: MWADUI FC 1-0 MBAO FC (VPL - 30/04/2018)

Mwadui FC imepanda kutoka nafasi ya 12 hadi ya 9 kwenye msimamo baada ya kushinda bao 1-0 dhidi ya Mbao FC kwenye mechi ya Ligi Kuu soka Tanzania Bara iliyochezwa leo jioni Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga. Bao pekee la Mwadui FC limefungwa dakika ya 29 na Charles Ilanfya aliyetumia vyema makosa ya golikipa Mussa Mohamed wa Mbao FC ambaye alipiga kimakosa mpira aliombabatiza mchezaji wa Mwadui FC, Salim Khamis. Hata hivyo, Mwadui walilazimika kucheza pungufu kwa dakika 38 za kipindi cha pili kutokana na golikipa wake, Anord Massawe kuoneshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja kufuatia kuudaka mpira nje ya eneo lake akiwa mchezaji wa mwisho.



FULL SHANGWE! Mashabiki wa Lipuli Baada ya Bao la Kwanza
FULL SHANGWE! Mashabiki wa Lipuli Baada ya Bao la Kwanza

FULL SHANGWE Mashabiki wa Lipuli Baada ya Bao la Kwanza Kikosi cha Simba kimeshindwa kupata alama tatu na badala yake kimepoteza pointi mbili katika Uwanja wa Samora mjini Iringa dhidi ya Lipuli, mchezo wa Ligi Kuu Bara. Mchezo huo ulioanza kwa kasi zaidi kwa wenyeji wakionesha kuumiliki mpira zaidi ya Simba, walikuwa wa kwanza kujiandikia bao mnamo dakika ya 31 ya kipindi cha kwanza kupitia Adam Salamba. Bao lilidumu kipindi cha kwanza ambapo mpaka Mwamuzi anapuliza kipyenga kwenda mapumziko, Lipuli walikuwa mbele kwa bao moja. Kipindi cha pili Simba walijitahidi kuamka na kuanza kujibu mapigo baada ya Kocha, Pierre Lechantre kufanya mabadiliko ya kumtoa beki Juuko Murushid, na nafasi yake ikichukuliwa na Mshambuliaji, Mburundi, Laudit Mavugo. Simba ilifanikiwa kupata bao la kusawazisha dakika ya 66 ya kipindi cha pili baada ya mpira wa kona kumfikia Mavugo ambaye aliumalizia kwa mguu na kufanya matokeo mpaka dakika 90 zinamalizika yaende sare ya 1-1. Matokeo hayo yameipa Simba alama moja na kuifanya ifikishe pointi 59 kwenye msimamo wa ligi. Install #GlobalPublishersApp Android: http://bit.ly/2AAQe1d iOS: http://apple.co/2Assf4M Subscribe http://www.youtube.com/c/uwazi FACEBOOK: https://www.facebook.com/Globalpublis... TWITTER: https://twitter.com/GlobalHabari Visit https://globalpublishers.co.tz/, Subscribe http://www.youtube.com/c/uwazi1 kupata video nyingine za aina hii, subscribe kwenye chanell yetu kwa kubofya… http://www.youtube.com/c/uwazi1 http://www.youtube.com/c/uwazi1 http://www.youtube.com/c/uwazi1 WEBSITE: https://globalpublishers.co.tz/ FACEBOOK: https://www.facebook.com/Globalpublis...



MAGOLI Yote ya Simba Vs Mbeya City 3 - 1
MAGOLI Yote ya Simba Vs Mbeya City 3 - 1

MAGOLI Yote ya Simba Vs Mbeya City 3 - 1 Kikosi cha Simba kimezidi kujikita kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Mbeya City FC. Mabao ya Simba yamefungwa na Emmanuel Okwi, Asante Kwasi na John Bocco. Mbeya City wamejipatia bao lao kupitia kwa Frank Ikobel na kuufanya mchezo umalizike kwa idadi hiyo ya mabao. Simba wamefikisha alama 55 dhidi ya watani wao wa jadi Yanga walio na 47. Mpaka sasa Simba imeshacheza jumla ya michezo 23 huku Yanga ikiwa na 22. Install #GlobalPublishersApp Android: http://bit.ly/2AAQe1d iOS: http://apple.co/2Assf4M Subscribe http://www.youtube.com/c/uwazi FACEBOOK: https://www.facebook.com/Globalpublis... TWITTER: https://twitter.com/GlobalHabari Visit https://globalpublishers.co.tz/, Subscribe http://www.youtube.com/c/uwazi1 kupata video nyingine za aina hii, subscribe kwenye chanell yetu kwa kubofya… http://www.youtube.com/c/uwazi1 http://www.youtube.com/c/uwazi1 http://www.youtube.com/c/uwazi1 WEBSITE: https://globalpublishers.co.tz/ FACEBOOK: https://www.facebook.com/Globalpublis... T



FULL HIGHLIGHTS: YANGA SC 3-1 STAND UNITED - VPL 12/03/2018
FULL HIGHLIGHTS: YANGA SC 3-1 STAND UNITED - VPL 12/03/2018

Hatimaye Yanga imefanikiwa kuwashika mahasimu wake Simba SC kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL) kwa kufikisha pointi 46, huku ikiendelea kubaki nafasi ya pili kwa tofauti ya mabao, licha ya Simba kuwa na kiporo cha mchezo mmoja mkononi. Yanga imefanikiwa kufikia hatua hiyo baada ya kuichapa Stand United kutoka Shinyanga jumla ya mabao 3-1 katika mchezo wa raundi ya 22 wa ligi hiyo uliopigwa leo kwenye dimba la Taifa jijini Dar es Salaam. Magoli ya Yanga yamefungwa na Ally Ally likiwa ni la kujifunga dakika ya 7, Ibrahim Ajib dakika ya 12 na Obrey Chirwa dakika ya 85 wakati bao pekee la Stand likifungwa na Vitalis Mayanga dakika ya 82. Hata hivyo Stand United watajilaumu wenyewe kwa kupoteza nafasi za wazi zaidi ya tano kwa washambuliaji wake kutokuwa makini kila wanapofika langoni kwa Yanga. Tazama kwa ufupi jinsi mambo yalivyokuwa.




« Previous Next »


Popular Tags

#Boston Celtics  #Football Defensive Skills  #Sergio Aguero  #Kyrie Irving  #Manuel Neuer  #Goalkeeper Saves  #Best Ball Controls  #Cristiano Ronaldo  #Neymar  #Franck Ribery  

Popular Users

#PMOIndia  #billsimmons  #b_ryan9  #KylieJenner  #RobGronkowski  #richarddeitsch  #jadande  #justinbieber  #JohnCena  #ladygaga  #TimTebow  #RealSkipBayless  #Cristiano  #MichelleDBeadle