Meneja Habari na Mawasiliano wa Yanga SC,Ally kamwe amewasili Dodoma kwa ajili ya mchezo wa kombe la Shirikisho la Benki ya CRDB,utakaochezwa Saa 2:00 usiku,Uwanja wa Jamhuri.
Leo Machi 29,2024 Mnyama Simba SC anashuka Dimba la Benjamin Mkapa kumenyana na Al Ahl kutoka Misri katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa robo fainali ya ligi ya Mabingwa Afrika,Saa 3:00
Mtangazaji Mwandamizi wa soka nchini, Baraka Adson Lamsi Mpenja, maarufu Mwamba wa Umalila, Fahari ya Itete, Sauti ya Radi, amekutana na kufanya Mazungumzo maalumu na Watangazaji vinara wa kandanda kutoka Azam Media LTD, Gharib Mzinga na Ayubu Hinjo. Wamezichambua mechi za robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Machi 29, Simba vs Al Ahly na Machi 30, Yanga vs Mamelodi Sundowns.
Mtangazaji kinara wa soka nchini, Baraka Mpenja, amefanya mazungumzo na Mtangazaji wa soka wa Azam Media LTD, Gharib Mohamed Ally Mzinga kuhusu Maisha yake ya nyuma lakini pia ikumbukwe leo ni kumbukizi ya kuzaliwa ya Mtangazaji machachari wa Soka Ghalibu Mzinga. Lakini pia Ghalibu mzinga ametoa mtazamo wake katika mechi ya ligi ya mabingwa Afrika kati ya Simba na Yanga kuwa zinaweza kufika hatua ya fainali katika mashindano hayo.
Meneja Habari na Mawasiliano wa Yanga SC,Ally kamwe aeleza namna ambavyo wamewapokea wapinzani wao Mamelodi Sundowns kwenye robo fainali ya ligi ya Mabingwa Afrika na namna wanavyojipanga kumenyana nao Machi 30,2024 Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Leo Machi 6,2024 Mnyama Simba anashuka Dimba la Jamhuri Morogoro kumenyana na Wajelajela Tanzania Prisons katika mchezo wa ligi kuu ya NBC ,Saa 10:00 jioni.
Mtangazaji kinara wa soka nchini, Baraka Mpenja, amefanya mazungumzo na Mtangazaji wa soka wa Azam Media LTD, Gharib Mohamed Ally Mzinga kuhusu mechi ya YANGA SC vs CR Belouizdad. Mzinga ndiye alitangaza mchezo huu ambayo Yanga wameshinda 4-0 na kufuzu Robo Fainali Ligi ya Mabingwa Afrika.
Kikosi cha Yanga SC kimefanya mazoezi yao ya mwisho katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kwa ajili ya Mchezo wa Februari 24,2024 wa ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi dhidi ya CR Belouizdad,Utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa,Saa 1:00 jioni.