Mtangazaji kinara wa soka nchini, Baraka Mpenja, amefanya mazungumzo na Mtangazaji wa soka wa Azam Media LTD, Gharib Mohamed Ally Mzinga kuhusu Maisha yake ya nyuma lakini pia ikumbukwe leo ni kumbukizi ya kuzaliwa ya Mtangazaji machachari wa Soka Ghalibu Mzinga. Lakini pia Ghalibu mzinga ametoa mtazamo wake katika mechi ya ligi ya mabingwa Afrika kati ya Simba na Yanga kuwa zinaweza kufika hatua ya fainali katika mashindano hayo.