Hii ni Soka Kijiweni ya tarehe 6/8/2018 ambapo Dodi alitembelea mji wa Morogoro na kukutana na kipaji cha soka kilichowahi kutamba katika vilabu vya Simb, Coastal Union, Mtibwa Sugar na sasa kiko Singida United United. Moja ya jambo lililofichuka mtaani kwake kutoka kwa washkaji zake ni historia ya beki huyo kula kuku, ambapo imeelezwa kuwa huyo jamaa ni mtaalamu wa kula miguu na vichwa vya kuku. Soka Kijiweni ni kila Jumatatu saa 1:00 Usiku, Azam Sports 2.
Zikiwa zimebaki wiki mbili kamili kufanyika kwa fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports, Azam TV imetia nanga mkoani Morogoro yaliko makao makuu ya timu ya Mtibwa Sugar ambayo itacheza dhidi ya Singida United. Akiwa huko ametembelea kituo cha soka cha Moro Youth ambacho kinazalisha wachezaji na kuwapeleka Mtibwa Sugar. Uongozi wa Moro Youth umeileza Azam TV kuwa watafurahi sana endapo Mtibwa itachukua kombe hilo kwani ni heshima kubwa kwao.
Timu ya Mtibwa Sugar imekubali kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Lipuli FC mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa leo kwenye dimba la Manungu, Morogoro. Mabao yote ya Lipuli yamefungwa na Seif Abdallah Karihe dakika ya 17 na 71, huku la Mtibwa likifungwa na Riffat Khamis dakika ya 53..
Mtibwa Sugar ya Morogoro, imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji Stand United katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC) uliopigwa leo kwenye dimba la Kambarage, Shinyanga. Mabao yote ya Mtibwa yamefungwa na Hassan Dilunga.
Simba Sc imeongeza kasi kulikimbilia taji la ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya ushindi wa 3-1 dhidi ya Mbeya City Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jioni ya leo. Ushindi huo unawafanya Wekundu hao wa Msimbazi wafikishe pointi 55 baada ya kucheza mechi 23, moja zaidi ya mabingwa watetezi, Yanga SC wenye pointi 47 katika nafasi ya pili. Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Hance Mabena wa Tanga aliyesaidiwa na Jesse Erasmo wa Morogoro na Rashid Zongo wa Iringa, hadi mapumziko Simba SC walikuwa tayari wamekwishavuna ushindi huo wa mabao 3-1.
Mechi imemalizika kwa ushindi mwembamba upande wa Simba licha ya kushambuliwa zaidi hasa dakika za mwisho kipindi cha pili. Mshambuliaji wa Simba Emmanuel Okwi ameifungia timu yake bao pekee la ushindi dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ukipigwa katika dimba la Jamhuri, Morogoro. Katika mchezo huo mgumu na uliokuwa na ushindani mkali, bao la Simba lilipatikana dakika ya 24 ambapo kinara huyo wa mabao aliunganisha pasi ya kichwa ya kutoka kwa John Bocco, baada ya kros ya Shiza Kichuya kutoka upande wa kushoto. Baada ya mchezo huo umati mkubwa ulionekana kujaa katikati ya dimba. Mchezo ulivyokuwa....
GOLI la Okwi Lililoipatia Simba Ushindi, Simba 1- 0 Mtibwa Sugar Simba SC imeendelea kujikusanyia alama katika Ligi Kuu Bara baada ya kuilaza Mtibwa Sugar FC kwa bao 1-0 jioni hii kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro. Mchezo huo uliokuwa unaambatana na mvua iliyokuwa ikinyesha Uwanjani, ulishuhudiwa nyavu zikitikiswa mnamo dakika ya 24 ya kipindi cha kwanza na Emmanuel Okwi. Okwi alifunga bao hilo akimalizia kazi mpira wa kichwa kutoka kwa John Bocco na kufanya mchezo huo udumu kwa dakika zote 90 huku matokeo yakisalia kuwa 1-0. Matokeo hayo yanaifanya Simba izidi kujikita kileleni kwa kufikisha alama 52 dhidi ya watani wao wa jadi Yanga wenye 46 mpaka sasa. Mechi inayofuatia kwa Simba itakuwa dhidi ya Wajelajela Mbeya City FC, itakayopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Install #GlobalPublishersApp Android: http://bit.ly/2AAQe1d iOS: http://apple.co/2Assf4M Subscribe http://www.youtube.com/c/uwazi FACEBOOK: https://www.facebook.com/Globalpublis... TWITTER: https://twitter.com/GlobalHabari Visit https://globalpublishers.co.tz/, Subscribe http://www.youtube.com/c/uwazi1 kupata video nyingine za aina hii, subscribe kwenye chanell yetu kwa kubofya… http://www.youtube.com/c/uwazi1 http://www.youtube.com/c/uwazi1 http://www.youtube.com/c/uwazi1 WEBSITE: https://globalpublishers.co.tz/ FACEBOOK: https://www.facebook.com/Globalpublis... TWITTER
Mshambuliaji wa Simba Emmanuel Okwi ameifungia timu yake bao pekee dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa ligi Kuu Tanzania Bara ukipigwa katika dimba la Jamhuri, Morogoro.