Content removal request!


MORO YOUTH CENTER: Mtibwa Sugar inakojipatia akina ‘Kichuya’

Zikiwa zimebaki wiki mbili kamili kufanyika kwa fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports, Azam TV imetia nanga mkoani Morogoro yaliko makao makuu ya timu ya Mtibwa Sugar ambayo itacheza dhidi ya Singida United. Akiwa huko ametembelea kituo cha soka cha Moro Youth ambacho kinazalisha wachezaji na kuwapeleka Mtibwa Sugar. Uongozi wa Moro Youth umeileza Azam TV kuwa watafurahi sana endapo Mtibwa itachukua kombe hilo kwani ni heshima kubwa kwao.