Content removal request!


MAGOLI: COASTAL UNION 2-0 AFRICAN LYON (TPL - 20/01/2019)

Wagosi wa Kaya timu ya Coastal Union imepata ushindi wa mabao 2-0 katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) uliopigwa leo kwenye Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga. Mabao ya Coastal Union waliokuwa wenyeji wa mchezo yamefungwa na Andrew Simchimba dakika ya 49 akimalizia mpira wa kurusha na Issa Abushehe dakika ya 90’+1 akimalizia pasi ya Haji Ugando.