Wagosi wa Kaya Coastal Union wakiwa na Alikiba aliyecheza kwa dakika 64, wamebanwa nyumbani na kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa kwenye Dimba la Mkwakwani Jijini Tanga. Coastal ndiyo waliotangulia kupata bao dakika ya 5 kupitia kwa Ayoub Lyanga aliyemalizia kwa kichwa kona iliyopigwa na Athuman Idd ‘Chuji’ ikitokana na jaribio la Alikiba. Mbeya City walipata bao la kusawazisha dakika ya 50 baada ya beki wa Coastal Union Bakari Mwamnyeto kujifunga akiwa katika jaribio la kuokoa.