Mbao FC imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons, katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. Bao hilo pekee limepatikana katika dakika ya nne kati ya dakika tano za nyongeza kupitia kwa mshambuliaji wake Ndaki Robert. Hili hapa bao lenyewe.
Simba SC 'yafumua' mfumo wa kikosi ili kuwakabili Mwadui FC hapo kesho kwenye dimba la Kambarage mkoani Shinyanga: Watafuta machungu waliyopewa na Mbao FC? Yanga SC kuendelea za wimbi la ushindi Dar? Azam FC je, suluhu zitaendelea ugenini? Kwa haya na mengine mengi ya kimichezo ungana na Ahmed Abdallah katika MSHIKEMSHIKE VIWANJANI.
Baada ya kupoteza mchezo wake wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara dhidi ya Mbao FC, mabingwa watetezi wa ligi hiyo, Simba SC leo wameendelea na mazoezi kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga wakisema wamerekebisha mfumo mzima wa kikosi chao ili waweze kushinda dhidi ya Mwadui FC kesho Jumapili Septemba 23, 2018 kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga. Meneja wa timu hiyo Abbas Ally anazungumzia marekebisho hayo.
Meneja wa timu ya Simba Abbas Ally amewataka wapenzi na mashabiki wa timu hiyo kutulia na kujiandaa na furaha katika mechi zijazo baada ya kufanya vibaya katika mechi mbili mfululizo. Abbas ametoa kauli hiyo mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati yao na Mbao FC uliomalizika kwa Simba kufungwa bao 1-0 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza leo Septemba 20, 2018. Amesema ligi siyo mashindano ya mtoano bali ina mechi mechi nyingi hivyo atakayemaliza vizuri ndiye atakaye kuwa bingwa, na Simba bado ina nafasi hiyo. Kuhusu mabadiliko ya Kocha wa timu hiyo kwenye safu ya ushambuliaji, Abbas amesema kocha anapanga kikosi kulingana na jinsi wachezaji walivyofanya mazoezi na mchezaji atakayeonekana kuwa vizuri zaidi ndiye anayepewa nafasi kwenye mechi. Kwa upande wake beki wa Simba ambaye pia ni nahodha msaidizi wa timu hiyo Mohamed Hussein 'Zimbwe Jr' amewataka mashabiki wa timu hiyo wasikate tamaa baada ya kufungwa na Mbao FC.
Subscribes:https://www.youtube.com/c/KidaniStars Ratiba ya mechi 11 zijazo za timu ya Simba, ratiba inaonesha mechi 5 mfululizo itazipiga kwenye Uwanja wake wa nyumbani. Ndanda FC v Simba SC Mbao FC v Simba SC Mwadui FC v Simba SC Simba SC v Biashara United Simba SC v Yanga SC Simba SC v African Lyon Simba SC v Stand United Simba v Alliance FC Ruvu Shooting FC v Simba SC JKT Tanzania v Simba SC KMC FC vs Simba SC Subscribes:https://www.youtube.com/c/KidaniStars
Msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) 2018/19 umeanza kwa lawama lukuki kwa waamuzi katika baadhi ya michezo wakidaiwa kukataa magoli ya timu mbalimbali kwa madai kuwa wafungaji walikuwa wameotea. Baadhi ya mechi zilizolalamikiwa ni ile ya Yanga vs Mtibwa Sugar, Coastal Union Vs Biashara United, Ruvu Shooting vs KMC na Alliance vs Mbao FC ikiwa ni raundi mbili pekee zimeshachezwa tangu kuanza kwa msimu huo. Suala hilo la kutafsiri sharia ya ‘off-side’ linachambuliwa kwa kina na Osman Kazi kupitia kipindi cha Kipyenga cha Mwisho cha wiki hii, Alhamisi Agosti 30, 2018. Kipyenga cha mwisho ni kila Alhamisi, saa 1:00 usiku LIVE Azam Sports 2.
Timu ya Mbao FC ya jijini Mwanza imepanda hadi nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa ligi kuu soka Tanzania bara baada ya kufanikiwa kutoa suluhu na Singida United katika mchezo uliopigwa jioni ya leo kwenye dimba la Namfua mkoani Singida. Singida United ambao walikuwa nyumbani wakisaka ushindi ambao utawasaidia kuweka katika nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi walijikuta katika wakati mgumu dhidi ya walinzi wa timu ya Mbao FC waliokuwa wakiondosha hatari zilizokuwa zikielekezwa langoni mwao. Matokeo hayo yamekuwa mazuri kwa upande wa Mbao FC waliokuwa ugenini kwa kuwa wamefikisha alama 7 na kuwa nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa ligi kuu baada ya kushinda michezo miwili na kutoa suluhu mchezo mmoja. Wakati Singida United katika michezo mitatu ya ligi waliocheza Namfua msimu huu wamefanikiwa kushinda mchezo mmoja, kupoteza mchezo mmoja na suluhu mchezo mmoja.
Ni muda mfupi kabla ya Derby ya Mwanza Alliance vs Mbao FC, ikiwa ni miongoni mwa mechi za kwanza katika msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara. Wawakilishi wa timu hizo wanashutumiana kufanyiana vitendo wanavyoamini kuwa ni vya kishirikiana katika vyumba vya kubadilishia nguo. Mechi inaanza saa 10:00 jioni na itakuwa LIVE #AzamSportsHD #AllianceVsMbao #TPL