Content removal request!


Utetezi wa Simba baada ya kuchapwa 1-0 na Mbao FC, Mwanza (TPL - 20/09/2018)

Meneja wa timu ya Simba Abbas Ally amewataka wapenzi na mashabiki wa timu hiyo kutulia na kujiandaa na furaha katika mechi zijazo baada ya kufanya vibaya katika mechi mbili mfululizo. Abbas ametoa kauli hiyo mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati yao na Mbao FC uliomalizika kwa Simba kufungwa bao 1-0 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza leo Septemba 20, 2018. Amesema ligi siyo mashindano ya mtoano bali ina mechi mechi nyingi hivyo atakayemaliza vizuri ndiye atakaye kuwa bingwa, na Simba bado ina nafasi hiyo. Kuhusu mabadiliko ya Kocha wa timu hiyo kwenye safu ya ushambuliaji, Abbas amesema kocha anapanga kikosi kulingana na jinsi wachezaji walivyofanya mazoezi na mchezaji atakayeonekana kuwa vizuri zaidi ndiye anayepewa nafasi kwenye mechi. Kwa upande wake beki wa Simba ambaye pia ni nahodha msaidizi wa timu hiyo Mohamed Hussein 'Zimbwe Jr' amewataka mashabiki wa timu hiyo wasikate tamaa baada ya kufungwa na Mbao FC.