Alichosema KOCHA SIMBA, Kotei, Chama, Mkwakwani Tanga
Alichosema KOCHA SIMBA, Kotei, Chama, Mkwakwani Tanga

Mambo mawili yaliyofungwa na Meddie Kagere katika dakika za 11 na 38 kipindi cha kwanza yameiwezesha Simba kung'ara kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya JKT Tanzania. Katika mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa CCM Mkwakwani Tanga, Simba ilimuazisha kiungo wake Mghana, James Kotei ambaye alikuwa anatumikia adhabu kufuatia kumpiga Gadiel Michael katika mechi ya mwisho iliyowakutanisha watani wa jadi. Ushindi huo unaifanya Simba kuendelea kuikimbiza Azam FC iliyo na pointi 27 kileleni kwa kufikisha alama 26. Licha ya ushindi huo, Kocha Patrick Aussems ameulalamikia Uwanja wa Mkwakwani kuwa si rafiki kwa kuchezea na akiomba kama kuna uwezekano uweze kufanyiwa ukarabati. #JKTTanzania #SIMBASC #MeddieKagere



MAGOLI YANGA  VS MBAO FC 2-0
MAGOLI YANGA VS MBAO FC 2-0

#YANGAvsMBAO MAGOLI YANGA VS MBAO FC 2-0 Yanga imefanikiwa kuapata ushindi wa 2-0 dhidi ya Mbao FC katika uwanja wa Taifa Dar es salaam. Bao la kwanza limepachikwa kimiani na Rafel Daud mnamo dakika ya 16 ya kipindi cha kwanza kwa njia ya kichwa kutokana na mpira wa adhabu uliopigwa na Ibrahim Ajibu. Baada ya kipindi cha kwanza kumalizika, kipindi cha pili Mbao walijitahada kuja kwa kasi kushambulia lango la Yanga lakini haikuweza kusaidia kitu. Licha ya mashambulizi hayo, Mbao FC walipata nafasi zingine kama nne kipindi cha kwanza lakini walishindwa kuzitumia vema. Zikiwa zimeongezwa dakika tano, Ibrahim Ajibu alifanikiwa kuingia kambani kwa kufunga bonge la bao kwa tikitaka ya aina yake na kuifanya Yanga iwe mbele kwa mabao 2-0. Mpaka dakika 90 zinamalizika, Yanga 2 na Mbao FC 0. Matokeo hayo yanaifanya Yanga kufikisha alama 16 katika msimamo wa ligi huku Mbao ikisalia na alama zake 14 kwenye nafasi ya 5. GlobalPublishersApp Android: http://bit.ly/2AAQe1d iOS: http://apple.co/2Assf4M Subscribe http://www.youtube.com/c/uwazi FACEBOOK: https://www.facebook.com/Globalpublis... TWITTER: https://twitter.com/GlobalHabari Visit https://globalpublishers.co.tz/, Subscribe http://www.youtube.com/c/uwazi1 Kupata video nyingine za aina hii, subscribe kwenye chanell yetu kwa kubofya… http://www.youtube.com/c/uwazi1 http://www.youtube.com/c/uwazi1 http://www.youtube.com/c/uwazi1 WEBSITE: https://globalpublishers.co.tz/ FACEBOOKInstall



HIGHLIGHT SIMBA VS AZAM FC 1-2 KAGAME CUP
HIGHLIGHT SIMBA VS AZAM FC 1-2 KAGAME CUP

HIGHLIGHT SIMBA VS AZAM FC 1-2 KAGAME CUP TIMU ya Azam FC imefanikiwa kutetea taji lake la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, maarufu kama Kombe la Kagame baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Simba SC jioni ya leo Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam. Shujaa wa Azam FC hii leo alikuwa ni Nahodha na beki, Aggrey Morris Ambroce aliyefunga bao la ushindi dakika ya 80 kwa shuti kali la mpira wa adhabu kutoka umbali wa mita 30, baada ya kumchungulia kipa Deogratius Munishi ‘Dida’. Katika mchezo huo uliokuwa mkali na wa kusisimua, Azam FC ilitangulia kwa bao la mshambuliaji wake hodari, Shaaban Iddi Chilunda dakikaya 33 ambaye leo alikuwa anacheza mechi ya mwisho kabla ya kwenda kuanza kuutumikia mkataba wa mkopo Tenerife ya Daraja la Kwanza Hispania. Install GlobalPublishersApp Android: http://bit.ly/2AAQe1d iOS: http://apple.co/2Assf4M Subscribe http://www.youtube.com/c/uwazi FACEBOOK: https://www.facebook.com/Globalpublis... TWITTER: https://twitter.com/GlobalHabari Visit https://globalpublishers.co.tz/, Subscribe http://www.youtube.com/c/uwazi1 Kupata video nyingine za aina hii, subscribe kwenye chanell yetu kwa kubofya… http://www.youtube.com/c/uwazi1 http://www.youtube.com/c/uwazi1 http://www.youtube.com/c/uwazi1 WEBSITE: https://globalpublishers.co.tz/ FACEBOOK: https://www.facebook.com/Globalpublis... TWITTER: https://twitter.com/GlobalHabari INSTAGRAM: https://www.instagram.com/globalpubli..



MKUDE Nje Kikosini Kuivaa Lipuli FC Kisa Hiki Hapa
MKUDE Nje Kikosini Kuivaa Lipuli FC Kisa Hiki Hapa

MKUDE Nje Kikosini Kuivaa Lipuli FC Kisa Hiki Hapa Kiungo wa klabu ya Simba, Jonas Mkude, ataukosa mchezo wa Simba dhidi ya Lipuli FC utakaopigwa mjini Iringa Aprili 21 2018, Jumamosi ya wiki hii. Mkude atakosekana katika mechi hiyo sababu atakuwa anatumikia adhabu ya kadi tatu za njano ambazo kwa mujibu wa kanuni, mchezaji hukosa mechi moja inayofuatia pindi anapofikisha idadi hiyo ya kadi. Simba itasafiri kuelekea Iringa wiki hii kwa ajili ya mchezo huo utakaopigwa Uwanja wa Samora. Kikosi hicho kitakuwa kinacheza na Lipuli kikiwa na harakati za kuwania ubingwa wa ligi ambao umekosekana Msimbazi kwa takribani miaka mitano. Install #GlobalPublishersApp Android: http://bit.ly/2AAQe1d iOS: http://apple.co/2Assf4M Subscribe http://www.youtube.com/c/uwazi FACEBOOK: https://www.facebook.com/Globalpublis... TWITTER: https://twitter.com/GlobalHabari Visit https://globalpublishers.co.tz/, Subscribe http://www.youtube.com/c/uwazi1 kupata video nyingine za aina hii, subscribe kwenye chanell yetu kwa kubofya… http://www.youtube.com/c/uwazi1 http://www.youtube.com/c/uwazi1 http://www.youtube.com/c/uwazi1 WEBSITE: https://globalpublishers.co.tz/ FACEBOOK: https://www.facebook.com/Globalpublis... T



SINGIDA UNITED 0-3 MTIBWA SUGAR, VPL HIGHLIGHTS (06/04/2018)
SINGIDA UNITED 0-3 MTIBWA SUGAR, VPL HIGHLIGHTS (06/04/2018)

Katika mchezo huo uliokuwa mbashara Azam Sports 2, Mtibwa Sugar ikiwa katika ubora wake, imeitandika Singida United magoli 3-0. Magoli ya Mtibwa yamefungwa na Kelvin Sabato ‘Kiduku’ aliyefunga goli la kwanza kwa mpira wa adhabu ndogo (free kick) dakika ya 22 ya mchezo na hadi kipindi cha kwanza kinamalizika, Mtibwa walikuwa mbele kwa bao hilo. Kipindi cha pili kilianza kwa Mtibwa kuzidisha moto langoni kwa Singida na hatimaye kupata bao la pili dakika ya 53 kupitia kwa Salum Kihimbwa akimlizia pasi ya Hassan Dilunga, huku Dilunga mwenyewe akiweka wavuni bao la tatu kwa mkwaju wa penati dakika ya 71.



FULL HIGHLIGHTS: MWADUI 2-2 SIMBA SC (15/02/2018)
FULL HIGHLIGHTS: MWADUI 2-2 SIMBA SC (15/02/2018)

Baada ya dakika 540 bila kuruhusu bao kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL), hatimaye vinara wa ligi hiyo, Simba wameruhusu nyavu zao kuguswa na vijana wa Mwadui FC ya Shinyanga. Mechi hiyo imepigwa katika dimba la Kambarage Shinyanga na kumalizika kwa sare ya mabao 2-2 na hivyo kuvunja rekodi ya nyavu za Simba kutoguswa, ambapo mara ya mwisho Simba kuruhusu bao ilikuwa Novemba 26 mwaka jana, kwenye mchezo dhidi ya Lipuli ambapo Asante Kwasi alifunga kwa mkwaju wa adhabu ndogo. Mabao ya Simba yamefungwa na John Bocco dakika ya 9 naEmmanuel Okwi dakika ya 71 huku Mabao ya Mwadui yakifungwa na David Luhende dakika ya 60 na Paul Nonga dakika ya 89



KOCHA GENDARMARIE; Nilijua Simba Watanifunga 10 Kumbe 4G!!
KOCHA GENDARMARIE; Nilijua Simba Watanifunga 10 Kumbe 4G!!

KOCHA GENDARMARIE; Nilijua Simba Watanifunga 10 Kumbe 4G!! SIMBA SC imeanza vyema michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Gendarmarie Tnare jioni ya leo Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam. Kwa ushindi huo uliotokana na mabao ya wazawa, kiungo Said Hamisi Ndemla, Nahodha na mshambuliaji John Raphael Bocco na mshasmbulaiji Mganda, Emmanuel Arnold Okwi – wazi Simba itakuwa na kazi nyepesi kwenye mchezo wa marudiano wiki mbili zijazo Djibouti. Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Alier Michael James aliyesaidiwa na Abdallah Suleiman Gassim na Gasim Madir Dehiya washika vibendera, Simba SC ilikwenda kupumzika ikiwa inaongoza kwa mabao 3-0. Kiungo Said Ndemla alizindua shangwe za mabao Simba SC dakika ya kwanza tu baada ya kufunga kwa shuti la kiufundi la mpira wa adhabu kutoka umbali wa mita 20, kufuatia Bocco kuchezewa rafu. Bocco akaifungia Simba SC bao la tatu dakika ya 32 kwa kichwa, akitumia mwanya wa kipa wa GendarmerieTnare kuanguka katika harakati za kuokoa. Mshambuliaji wa zamani wa Azam FC, Bocco akafunga bao la tatu dakika ya 45 kwa kichwa tena akimalizia pasi nzuri ya mshambuliaji mwenza, Mganda Emmanuale Okwi Subscribe muda huu www.youtube.com/user/uwazi1 Install #GlobalPublishersApp Android: http://bit.ly/2AAQe1d iOS: http://apple.co/2Assf4M Subscribe http://www.youtube.com/c/uwazi FACEBOOK: https://www.facebook.com/Globalpublis... TWITTER: https://twitter.com/GlobalHabari Visit https://globalpublishers.co.tz/, Subscribe http://www.youtube.com/c/uwazi1 Kupata video nyingine za aina hii, subscribe kwenye chanell yetu kwa kubofya… http://www.youtube.com/c/uwazi1 http://www.youtube.com/c/uwazi1 http://www.youtube.com/c/uwazi1 WEBSITE: https://globalpublishers.co.tz/ FACEBOOK: https://www.facebook.com/Globalpublis... TWITTER: https://twitter.com/GlobalHabari INSTAGRAM: https://www.instagram.com/globalpubli..



OKWI HUYU HAPA:ATUMA SALAMU MECHI IJAYO YA KAGERA SUGAR
OKWI HUYU HAPA:ATUMA SALAMU MECHI IJAYO YA KAGERA SUGAR

Please watch: "MAGOLI YOTE YA SIMBA 5 - 0 MBAO" https://www.youtube.com/watch?v=lU7L3hP4BP0 --~-- MSHAMBULIAJI Mganda Emmanuel Arnord Okwi ametokea benchi na kufunga mabao mawili Simba SC ikishinda 4-0 dhidi ya Singida United katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Matokeo hayo yanaifanya Simba SC ifikishe pointi 29, baada ya kucheza mechi 13, ikiwazidi pointi saba mabingwa watetezi, Yanga SC na pointi mbili Azam FC wenye 27 katika nafasi ya pili, wakati Mtibwa Sugar sasa ni ya tatu kwa pointi zae 24 baada ya timu zote kucheza mechi 13. Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Jacob Adongo wa Mara, aliyesaidiwa na Mohammed Mkono wa Tanga na Gasper Ketto wa Arusha hadi mapumziko Simba SC walikuwa wanaongoza kwa mabao 2-0. Kiungo Shiza Ramadhani Kichuya alianza kuifungia Simba SC dakika ya tatu akimalizia mpira wa adhabu uliopigwa na kiungo mkongwe Mwinyi Kazimoto, kufuatia John Raphael Bocco kuangushwa nje kidogo ya boksi. Singida wakacharuka na kuanza kupeleka mashambulizi mfululizo langoni mwa Simba kusaka bao la kusawazisha, lakini ngome ya Wekundu wa Msimbazi ikiongozwa na Erasto Edward Nyoni ilikuwa imara kuondosha hatari zote. Beki Mghana, Asante Kwasi akaifungia Simba SC bao la pili dakika ya 25 akimvisha kanzu kipa Peter Manyika aliyetoka langoni bila hesabu nzuri baada ya pasi ndefu ya kiungo Said Ndemla aliyetokea benchi kuchukua nafasi ya Kazimoto. Bao hilo lilionekana kuwachanganya Singida United wanaofundishwa na kocha Mholanzi, Hans van der Pluijm na kuwaruhusu Simba kutawala zaidi mchezo huo. Kipindi cha pili, mashabiki wa Simba SC wakaripuka kwa shangwe baada ya kumuona kocha wao mpya, Mfaransa Pierre Lechantre aliyeongozana na msaidizi wakea, kocha wa viungo, Mmorocco Mohammed Aymen Hbibi jukwaa kuu. Kocha huyo amekuja kusaini mkataba wa kuifundisha Simba kuchukua nafasi ya Mcameroon, Joseph Marius Omog aliyeondolewa Desemba na atafanya kazi na Mrundi, Masudi Juma ambaye amekuwa akiiongoza tangu kipindi chote hiki. Okwi akatokea benchi dakika ya 65 kuchukua nafasi ya kiungo Muzamil Yassin na akafunga mabao mawili ndani ya dakika saba. Alifunga bao la tatu dakika ya 75 akimalizia pasi ya Shiza Kichuya na la nne dakika ya 82 akimalizia pasi ya Ndemla. Alifunga mabao hayo, baada ya kumsetia pasi nzuri Kichuya, akapiga nje akiwa ndani ya sita. Kikosi cha Simba SC leo kilikuwa; Aishi Manula, Nicholas Gyan, Asante Kwasi, Juuko Murshid, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, James Kotei/Mohammed Ibrahim dk88, Mwinyi Kazimoto/Said Ndemla dk22, John Bocco, Shiza Kichuyana Muzamil Yassin/Emmanuel Okwi dk65. Singida United; Peter Manyika, Michael Rusheshangoga, Shafiq Batambuze, Kennedy Wilson, Malik Antiri, Mudathir Yahya, Deus Kaseke, Tafadzwa Kutinyu/Yussuf Kagoma79, Lubinda Mundia/Kenny Ally76, Kambale Salita Gentil na Kiggi Makassy/Salum Chukwu dk62.




« Previous Next »


Popular Tags

#Cleveland Cavaliers  #Lionel Messi  #Russell Westbrook  #Goalkeeper Saves  #Mesut Ozil  #Kobe Bryant  #Best Goals  #Chris Paul  #Kevin Durant  #Best Football Defending Skills  

Popular Users

#MikePereira  #espn  #kobebryant  #Harry_Styles  #CNN  #BaileyLAKings  #cesc4official  #SportsCenter  #taylorswift13  #DanicaPatrick  #SteveNash  #sportspickle  #ArianFoster  #MieshaTate