Content removal request!


FULL HIGHLIGHTS: MWADUI 2-2 SIMBA SC (15/02/2018)

Baada ya dakika 540 bila kuruhusu bao kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL), hatimaye vinara wa ligi hiyo, Simba wameruhusu nyavu zao kuguswa na vijana wa Mwadui FC ya Shinyanga. Mechi hiyo imepigwa katika dimba la Kambarage Shinyanga na kumalizika kwa sare ya mabao 2-2 na hivyo kuvunja rekodi ya nyavu za Simba kutoguswa, ambapo mara ya mwisho Simba kuruhusu bao ilikuwa Novemba 26 mwaka jana, kwenye mchezo dhidi ya Lipuli ambapo Asante Kwasi alifunga kwa mkwaju wa adhabu ndogo. Mabao ya Simba yamefungwa na John Bocco dakika ya 9 naEmmanuel Okwi dakika ya 71 huku Mabao ya Mwadui yakifungwa na David Luhende dakika ya 60 na Paul Nonga dakika ya 89