Baada ya dakika 540 bila kuruhusu bao kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL), hatimaye vinara wa ligi hiyo, Simba wameruhusu nyavu zao kuguswa na vijana wa Mwadui FC ya Shinyanga. Mechi hiyo imepigwa katika dimba la Kambarage Shinyanga na kumalizika kwa sare ya mabao 2-2 na hivyo kuvunja rekodi ya nyavu za Simba kutoguswa, ambapo mara ya mwisho Simba kuruhusu bao ilikuwa Novemba 26 mwaka jana, kwenye mchezo dhidi ya Lipuli ambapo Asante Kwasi alifunga kwa mkwaju wa adhabu ndogo. Mabao ya Simba yamefungwa na John Bocco dakika ya 9 naEmmanuel Okwi dakika ya 71 huku Mabao ya Mwadui yakifungwa na David Luhende dakika ya 60 na Paul Nonga dakika ya 89
#CRDBBankFederationCup: Tazama matukio yote muhimu yaliyojiri kwenye mchezo kati ya Simba dhidi ya TRA United kwenye mchezo wa robo fainali ya CRDB Bank Federation Cup. Magoli ya Simba yamefungwa na Clatous Chama, Anicet Oura, Selemani Mwalimu na Bashiri Kibaila. Mchezo wa nusu fainali ni Coastal Union dhidi ya Simba SC. FT: Simba SC 4-0 TRA United #KombeLaShirikishoLaCRDBBank #CRDBCup #FACup #SimbaSCVsTRAUnited #SimbaSC #TRAUnited #SimbaTRAUnited
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara, Yanga SC wamepoteza mchezo kwa mara ya kwanza msimu huu, wakichapwa 3-2 na Dodoma Jiji, mchezo, mchezo ukipigwa Airtel Stadium, Singida. Magoli ya Yanga yamefungwa na Allan Okello dakika ya 2 na 41, huku magoli ya Dodoma Jiji yakitoka kwa Bakari Mwamnyeto aliyejifunga dakika ya 29, Mwana Kibuta David dakika ya 90 na Wazir Junior Shemtembo dakika za nyongeza. Haya hapa magoli yote..
#NBCPL: Tazama magoli yote matano yaliyofungwa kwenye mchezo wa NBC Premier League kati TRA United dhidi ya Azam FC. FT: TRA United 4-1 Azam FC Magoli ya TRA United yamefungwa na Ally Ng'azi, Ammy Mapaka na Ramadhan Salum 'Chobwedo' Goli la Azam FC limefungwa na Jephte Kitambala Bola. #NBCPremierLeague #LigiKuuYaNBC #NBCPL #NBCPLUpdates #ImenogaZaidi #TRAUnitedvsAzamFC #TRAUnited #AzamFC #TRAUnitedAzamFC
KARIAKOO DERBY | Imepigwa dabi moja ya maana sana kwenye Dimba la Amaan, Zanzibar, Yanga na Simba wakimaliza dakika 90 bila bao, lakini burudani za kutosha. Hii ni mechi ya Ligi Kuu ya NBC Tanzania
Yanga SC imeichakaza JKT Tanzania mabao 5-0 katika mchezo wa ligi kuu ya NBC uliopigwa leo kwenye Dimba la KMC Complex, Dar es Salaam. Wafungaji wa magoli haya ni Mohamed Hussein Zimbwe Jr,, Aurellio Depu, Mudathir Yahya, Prince Dube na Shekhan Ibrahim.
Ni mechi ya kirafiki ya kalenda ya FIFA iliyopigwa kwenye Dimba la Al Salaam, Cairo nchini Misri, na timu ya taifa ya Tanzania #TaifaStars kuchwa 4-3 na Kuwait. Magoli ya Tanzania yamefungwa na M’mombwa 6’, 87’, na Taryin Allarakhia 34’ huku ya Kuwait yakitoka kwa Daham 46’, 52’ Nasser 63’ na Hamdan 69’
KMC vs SINGIDA BS: Kocha Marcio Maximo wa KMC, amesema mataifa ya Argentina na Brazil ni wapinzani ndani ya uwanja, ...
KARIAKOO DEEBY | Fahamu ukweli kuhusu matukio yote yaliyozua utata kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii kati ya Yanga na Simba uliopigwa Septemba 16, 2025. Moja kati ya matukio yaliyozua gumzo ni goli pekee walilofunga Yanga na kuamua mshindi wa Ngao ya Jamii 2025. Osman Kazi na jopo lake wanamaliza utata kwa kutumia sheria na kanuni za soka