KOCHA GENDARMARIE; Nilijua Simba Watanifunga 10 Kumbe 4G!! SIMBA SC imeanza vyema michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Gendarmarie Tnare jioni ya leo Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam. Kwa ushindi huo uliotokana na mabao ya wazawa, kiungo Said Hamisi Ndemla, Nahodha na mshambuliaji John Raphael Bocco na mshasmbulaiji Mganda, Emmanuel Arnold Okwi – wazi Simba itakuwa na kazi nyepesi kwenye mchezo wa marudiano wiki mbili zijazo Djibouti. Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Alier Michael James aliyesaidiwa na Abdallah Suleiman Gassim na Gasim Madir Dehiya washika vibendera, Simba SC ilikwenda kupumzika ikiwa inaongoza kwa mabao 3-0. Kiungo Said Ndemla alizindua shangwe za mabao Simba SC dakika ya kwanza tu baada ya kufunga kwa shuti la kiufundi la mpira wa adhabu kutoka umbali wa mita 20, kufuatia Bocco kuchezewa rafu. Bocco akaifungia Simba SC bao la tatu dakika ya 32 kwa kichwa, akitumia mwanya wa kipa wa GendarmerieTnare kuanguka katika harakati za kuokoa. Mshambuliaji wa zamani wa Azam FC, Bocco akafunga bao la tatu dakika ya 45 kwa kichwa tena akimalizia pasi nzuri ya mshambuliaji mwenza, Mganda Emmanuale Okwi Subscribe muda huu www.youtube.com/user/uwazi1 Install #GlobalPublishersApp Android: http://bit.ly/2AAQe1d iOS: http://apple.co/2Assf4M Subscribe http://www.youtube.com/c/uwazi FACEBOOK: https://www.facebook.com/Globalpublis... TWITTER: https://twitter.com/GlobalHabari Visit https://globalpublishers.co.tz/, Subscribe http://www.youtube.com/c/uwazi1 Kupata video nyingine za aina hii, subscribe kwenye chanell yetu kwa kubofya… http://www.youtube.com/c/uwazi1 http://www.youtube.com/c/uwazi1 http://www.youtube.com/c/uwazi1 WEBSITE: https://globalpublishers.co.tz/ FACEBOOK: https://www.facebook.com/Globalpublis... TWITTER: https://twitter.com/GlobalHabari INSTAGRAM: https://www.instagram.com/globalpubli..