Miamba hiyo ya soka inafikiria kumuachia Luis ili wapate nafasi ya kuvuta mchezaji mwingine wa kigeni na Simba baada ya kusikia taarifa hizo, fasta wakatuma maombi kwa Al Ahly kama ikiwezekana wamruhusu aje kukipiga tena Msimbazi. Simba inamtaka Luis kwa mkopo, lakini ikipanga kumpunguzia mshahara, kitu ambacho kwa sasa kinajadiliwa na miamba hiyo kuona inakuwaje. Taarifa kutoka ndani ya Simba zinasema kuwa katika ombi lao wamependekeza Luis apunguze mshahara kutoka Dola 50,000 (zaidi ya Sh 100 milioni) kwa mwezi na kuwa isiyozidi dola 15,000 (zaidi ya Sh 30 milioni). -- Dar24 ni chanzo namba moja cha habari kwa watanzania mahali popote walipo duniani. Kwa habari za uhakika kutoka nyanja mbali mbali. JE, NA WEWE UNA HABARI? ⚫️ WASILIANA NA DAR24 MEDIA: +255 679 979 786 ⚫️ Email: dar24newsroom@gmail.com ⚫️ Website: www.dar24.com ⚫️ Instagram: @Dar24news ⚫️ Facebook: @dar24 ⚫️ Twitter: @Dar24News #HAJIMANARA #AHMEDALLY #USAJILI
Usisahau ku "SUBSCRIBE" Channel yetu kwa habari nyinginezo nyingi na nzuri USHINDI WA SIMBA WAIPALIA YANGA/ MNYAMA NI BORA AFRIKA/ NI MAOMBI PEKEE KUIBAKISHA MTIBWA VPL? #BonaTV #Exclusive
SIMBA WANASUBIRI MAJIBU YA CAF KUHUSU KUINGIA MASHABIKI MCHEZO VS AS VITA APRIAL 3
#Simbasc#ALMerrikh#Maombi#CafOnline Klabu ya Simba imetuma maombi CAF kufanya uchunguzi kuhusu klabu ya Al Merreikh ya sudan kuwatumia wachezaji wawili waliofungiwa na shirikisho la mpira wa miguu la sudan wakati wa mchezo wao ulichezwa marchi 6 mwaka huu mjini khatoum . Wachezaji ambao waliojumuhishwa ni pamoja na Ramadhan ajab na bakhiet khamis ambao walifungiwa na chama cha soka sudan Sudan Football Association] kwa muda wa miezi sita kutokana na kila mmoja kua na mikataba na vilabu viwili tofauti.
Rais Magufuli ameahidi kutoa shilingi Milioni 20 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa ofisi ya wajasiriamali wa eneo la Feri katika Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam na ameahidi kufanyia kazi changamoto mbalimbali zinazowakabili katika shughuli zao. Ametoa ahadi hiyo leo alipokutana na wajasiriamali hao ambao wanajumuisha wavuvi wadogo na mamalishe wakati akiwa katika mazoezi ya jioni pamoja na mkewe Mama Janeth Magufuli ambaye pia amewachangia wajasiriamali wanawake shilingi Milioni 5. Pamoja na kumshukuru Mhe. Rais Magufuli, wajasiriamali hao wameomba awasaidie wasifukuzwe na Manispaa ya Ilala katika eneo hilo, na badala yake wawekewe utaratibu mzuri wa kufanya biashara zao. Pia wameomba waondolewe ushuru unaotozwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) kwa mitumbwi ya wavuvi wadogo wa samaki, kama ambavyo Serikali imewaondolea ushuru wakulima wanaopeleka sokoni mazao yasiyozidi tani moja. Aidha, Wajasiriamali hao wamempongeza Mhe. Rais Magufuli kwa kazi nzuri ya kuiongoza nchi na kushughulikia kero za Watanzania ikiwa ni pamoja na kuwatembelea na kuwasikiliza kwa mara ya pili. Kwa upande wake Mhe. Rais Magufuli ameahidi kufanyia kazi maombi ya Wajasiriamali hao na amewapongeza kwa juhudi zao za kujitafutia kipato.