Miamba hiyo ya soka inafikiria kumuachia Luis ili wapate nafasi ya kuvuta mchezaji mwingine wa kigeni na Simba baada ya kusikia taarifa hizo, fasta wakatuma maombi kwa Al Ahly kama ikiwezekana wamruhusu aje kukipiga tena Msimbazi. Simba inamtaka Luis kwa mkopo, lakini ikipanga kumpunguzia mshahara, kitu ambacho kwa sasa kinajadiliwa na miamba hiyo kuona inakuwaje. Taarifa kutoka ndani ya Simba zinasema kuwa katika ombi lao wamependekeza Luis apunguze mshahara kutoka Dola 50,000 (zaidi ya Sh 100 milioni) kwa mwezi na kuwa isiyozidi dola 15,000 (zaidi ya Sh 30 milioni). -- Dar24 ni chanzo namba moja cha habari kwa watanzania mahali popote walipo duniani. Kwa habari za uhakika kutoka nyanja mbali mbali. JE, NA WEWE UNA HABARI? ⚫️ WASILIANA NA DAR24 MEDIA: +255 679 979 786 ⚫️ Email: dar24newsroom@gmail.com ⚫️ Website: www.dar24.com ⚫️ Instagram: @Dar24news ⚫️ Facebook: @dar24 ⚫️ Twitter: @Dar24News #HAJIMANARA #AHMEDALLY #USAJILI